kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Nimepata kuwasikiliza wauguzi nikaona wana hoja nzito.
Baraza lao la Uuguzi ni rahisi sana kusababisha migomo Kwa wauguzi kutokana na kufanya maamuzi yasiyowashirikisha wauguzi wenyewe. Mfano, kujenga jengo kubwa Sana la Baraza bila kuonyesha ulazima wa kuwa na jengo kubwa kama hilo.
Kuchangisha na kupandisha viwango vya tozo mbalimbali Kwa wanafunzi, wauguzi na vyuo vya Uuguzi bila kushirikisha wadau na bila kujali kuwa viwango vya mishahara Kwa wauguzi havijapanda Kwa muda mrefu Kwa sababu zinazoeleweka.
Baraza linafahamu kuwa baada ya watumishi hewa kuondolewa vyuo na hospital zimepungukiwa na wauguzi hivyo kung'ang'ania wauguzi kufanya mitihani ya license Kwa Ada kubwa na malipo makubwa ya kupata leseni za Uuguzi kunapunguza wauguzi wanaostahiki kwenda kuwahudumia wagonjwa Kwa kukosa hela za kufanya mitihani hiyo na kulipia leseni. Hii inasababisha wananchi wengi kwenda kuhudumiwa na waganga na wakunga wa jadi mitaani.
Wasikilize wauguzi na pata maelezo ya kina kutoka Baraza lao kuhusu sababu hasa za kupandisha tozo mbalimbali kwenye kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu na wakati serikali imeelekeza nguvu nyingi kwenye ujenzi wa miradi mikubwa muhimu.
Ni hayo buana.