Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mazrui aipongeza MOI kwa huduma nzuri

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mazrui aipongeza MOI kwa huduma nzuri

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
214
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui ameipongeza Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kutoa huduma bora za matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kwa wanachi wa Zanzibar wanaotibiwa MOI.

Mhe. Mazrui ameyasema hayo leo Jumanne Mei 06, 2025 alipotembelea banda la MOI katika maonesho ya Wiki ya Afya Zanzibar, yanayofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar.

“ Naipongeza Taasisi ya MOI kwa kutoa matibabu bora kwa wananchi wa Zanzibar wanaokuja kutibiwa magonjwa ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika Taasisi yenu” amesema Mhe. Mazrui

Aidha, Mhe. Mazrui ameishukuru MOI kwa kushiriki katika maonesho hayo yaliyoanza tarehe 4 Mei ambayo yatafikia tamati 10 Mei 2025 Zanzibar.
IMG-20250506-WA0068.jpg
IMG-20250506-WA0065.jpg
IMG-20250506-WA0063.jpg
 
Back
Top Bottom