"waziri wa elimu akamatwe na ashitakiwe"... James mbatia

"waziri wa elimu akamatwe na ashitakiwe"... James mbatia

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KAWAMBWA.jpg


Baada ya Serikali kutoa kauli kuhusu mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka jana, Mbunge James Mbatia (NCCR-Mageuzi), ametaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, awajibike na ikiwezekana akamatwe na kushitakiwa.




Kauli hiyo aliitoa jana kwa waandishi wa habari akisema kuvurugika kwa utaratibu kutokana na kuanzisha utaratibu mpya wa usahihishaji na kutoa alama bila kushirikisha wadau, unamgusa Waziri ambaye ndiye mwenye dhamana.




Alisema watu wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) hawawezi kufanya uamuzi bila kujulikana na watu wengine wa juu akiwamo Waziri na kusababisha wanafunzi wengi kufeli mitihani ya kidato cha nne mwaka jana.


Aidha, Mbatia alisema kwa mantiki na falsafa ya utendaji haiwezekani utaratibu huo ukakosa baraka za Waziri wa Elimu.“Si kujiuzulu tu kuna watu wanatakiwa wakamatwe na kushitakiwa kwa kosa hili, kwa kuwa limefanyika kwa makusudi…limetengenezwa, halikutokea kwa bahati mbaya,” alisema.


Mbatia ambaye alifuatana na Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), alisema Dk Kawambwa alitakiwa kwa ripoti ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, asionekane hadharani kwa sababu ni aibu kwake.


Aidha, alisema Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kuchunguza kufeli kwa wanafunzi hao, imebeba asilimia 75 ya maudhui ya hoja yake aliyoiwasilisha bungeni kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini mwaka jana.

Aidha, alisema ni vema wanasiasa na watu wengine wakakubaliana na ukweli wa kusikiliza hoja na kuacha ushabiki wa kisiasa.


“Hatuwezi kusubiri Rais na Waziri Mkuu kuwa viranja wa kuhakiki mawazo yanayotolewa na wananchi. Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote kuleta mabadiliko . La msingi ni taarifa na si mtoa taarifa,” alisema na kuongeza:

“Hata mwendawazimu ana haki ya kusikilizwa. Kama hoja yangu ingelipokewa na Bunge, hatua kadhaa nilizopendekeza zingekuwa zimetekelezwa na Taifa lingejiepusha na aibu hii.”


Aidha, Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, alisema ripoti hiyo inaliamsha Bunge kutoka usingizi wa kutumia itikadi za vyama kufanya uamuzi.

Alisema aliyesoma au kusikiliza hoja yake, amethibitishiwa na ripoti ya Tume ya Waziri Mkuu kwamba misimamo ya kiitikadi bungeni ni adui wa maendeleo ya Taifa.
"WAZIRI WA ELIMU AKAMATWE NA ASHITAKIWE"... JAMES MBATIA - MPEKUZI HURU
 
Huku kwenye nchi zilizostaarabika viongozi huachia ngazi kwa hiari kuonesha kuwajibika, hapo kwetu tz naona utamaduni huu haujafika bado.
 
Huku kwenye nchi zilizostaarabika viongozi huachia ngazi kwa hiari kuonesha kuwajibika, hapo kwetu tz naona utamaduni huu haujafika bado.
Akiwajibika then awe reference iwe kwake kila mkijadili udhaifu wenu?mf leo kila mtu akizungumzia kufanya vibaya katika michezo,utashangaa eti wana m refer Mungai kwamba alifuta michezo!Ukizungumzia ufisadi hata wa halmashauri,mitanzania hii hii inasema Lowasa!Tatizo sio Waziri,tatizo ni sisi watanzania,wengi tunadhani tunajua ingawa ukweli ni kwamba ni wababaishaji wakubwa katika kila nyanja alafu uswahili na maneno maneno ya kutafuta kondoo wa kafara ndo jadi yetu.


Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ikiwa yeye binasi haoni sababu ya kujiuzulu basi aliyemteua anaweza kumfuta kazi ili kulinda heshima ya serikali na kuongeza imani ya wananchi kwenye utendaji wake.
 
tz ni nchi inayoendeshwa kwa matukio,hili litapita kisanii hivi hivi.ni upepo pia utapita....kisha kungoja lingine kubwa litakalo lifanya la Kawambwa na nduguze lionekane dogo.
 
Naunga mkono hoja 100% Ila kwa nchi yetu bosi wake anajua ni upepo utapita.
 
Back
Top Bottom