Waziri wa elimu (kawambwa) na naibu wake (mulugo) wajiuzulu

Waziri wa elimu (kawambwa) na naibu wake (mulugo) wajiuzulu

JOSE KASANO

Senior Member
Joined
Apr 23, 2013
Posts
122
Reaction score
95
Kutokana na kadhia na aibu kubwa ambayo Taaifa la Tanzania limeipata katika macho ya ulimwengu kwa kuutangazia umma kuwa zaidi ya wanafunzi wake waliohitimu kidato cha nne 2012 walipata sifuri halafu  baadaye ikatangazwa kuwa matokeo hayo yamefutwa na  yatatangazwa mengine  baada  ya kumaliza uchakachuaji, viongozi waandamizi wa wizara hii ya elimu Kawambwa  na Mulugo wanatakiwa kuachia ngazi mara moja maana hawana maana tena ya kuendelea kuongoza wizara hii.

Kinachosikitisha ni kwamba viongozi hawa wanajiona ni watu wenye weledi wa kutosha  mbele ya umma.Mulugo ni kilaza kila mtu anajua, tuanzie kwenye speech aliyotoa kule Afrika Kusini mbele ya Mataifa kuwa Tanzania ni muungano wa nchi za Zimbabwe, Tanganyika na pemba na kwamba muungano huo ulikuwa mwaka 11964.Huyu ni mtu ambaye ametuhumiwa kutumia vyeti vya wasomi wengine mpaka hapo alipo halafu anapewa eyi aongoze wasomi kama siyo dharau kwa Watanzania ni nini? Rais Kikwete una dharau kwa Watanzania waliokuamini na kukupa kura ili ukaongoze ncchi na kama unakerwa na kuchukia matatizo ya nchi hii HUNA BUDI KUWAONDOA KAWAMBWA NA MULUGO MARA MOJA,afadhali wizara ibaki bila waziri na naibu wake maana hata hawa unaoendelea kuwakodolea macho hawana mbele wala nyuma.Iwapo RAIS Kikwete hutaki kuwaondoa Watanzania kwa umoja wetu tutauangusha utawala wa chama chako  siku si nyingi za mbeleni kwa njia yoyote ile.

Leo mnatwambia eti Baraza la mawaziri limeridhia matokeo kufutwa, hivi mlitafaakari kwa kina kuangalia athari zake kweli? Mbona hamkuja na mikakati ya kufidia wanafunzi wote waliopata maafa? Mh.James Mbatia amependekeza Kawambwa kukamatwa na kugunguliwa mashtaka kwa kusababisha mauaji, NINAMUUNGA MKONO MIA KWA MIA.

>Vija wetu wamejiua baada ya kuwapachikia matokeo ambayo mlijua si ya kwao.
> Wazazi wengi wamekwigharamika kwa kuwapeleka tena shule za binafsi watoto wao, hivyo mnaendelea kuwatobia mifuko yao bila sababu ya msingi wala maana yoyote.
>Wapo wanafunzi ambao wameathirka kisaikolojia, bila aibu hamna hata chembe ya akili angalau kusema watoto muwafanyie counselling.
>Hamna mikakati ya kuboresha mishahara ya walimu ili walipwe kama watumishi wengine na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, mnakimbilia kuchakachua matokeo, mtachakachua kila mwaka?

RAI KWAKO RAIS KIKWETE VUNJA UKIMYA TUONDOLEENI  HIZO SANAMU WIZARANI labda tunaweza kupumua, KAWAMBWA NA MULUGO TUNAWAOGOPA ZAIDI YA MARADHI MWILINI, HAWAFAI! HAWAFAI! HAWAFAI! HAWASTAHILI! KAMA HIYO UNAONA NGUMU BASI ONDOKA WEWE MWENYEWE UTUACHIE NCHI YETU!

Sasa mbona HEADING na CONTENT yako havina uhusiano yaani nimekatiza usingizi nikajua kuna jipya limetokea kumbe yaleyale.

Big up Jose, hizo sanamu lazima ziondoke pamoja na Sanamu Kamishna Bhalalusesa

Back
Top Bottom