Waziri wa Elimu tunaomba uingilie kati vyeti vyetu Chuo cha Bandari, Tandika

Waziri wa Elimu tunaomba uingilie kati vyeti vyetu Chuo cha Bandari, Tandika

Magita

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2013
Posts
319
Reaction score
144
Tulimaliza Chuo tangu Nov, 2017.

Ilipofika June 2018 Vyeti vikagawiwa kwa Wahitimu wote, lakini katika Vyeti vile kulikuwa na makosa ya kukosewa majina baadhi ya Wahitimu, tukaambiwa na Mkuu wa Chuo kuwa wote ambao majina yetu yalikosewa yatupasa tujiorodheshe baada ya miezi mitatu tukachukue.

Tangu June 2018 hadi hii leo 13 Nov. 2019 hakuna vyeti, kila ukienda unaambiwa bado.

KATIKA AJIRA tunashindwa kuomba kazi katika Makampuni kwasababu hatuna vyeti, ndugu Waziri je hii ni haki?

Tumemaliza Diploma mwaka wa tatu sasa vyeti mpaka sasa hatujapewa.
 
Mkuu nendeni wizarani mkatoe malalamiko yenu.
 
Poleni sana nyote mliokumbwa na adha hiyo. Naamini ni uzembe wa kupindukia unaofanywa na ofisi husika.

Mamlaka husika ichukue hatua kali za kinidhamu dhidi ya wahusika wote ili kukomesha tabia hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni saana....

Mara nyingi issue za hivi huwa ni uzembe wa chuo husika. Kesi km izo nimeziona nyingi na sio hapo tu kuna chuo kipo ruvuma uko kinaitwa ST THOMAS ni ujinga mtupu... Nilimpeleka dogo.. Now ni mwez wa 8 hajapata cheti... kashndwa kuendelea na elimu ya juu.

Nimewasiliana na email ya nacte wamekausha km hawaioni, ukiwafata wao wanaleta majibu ya dharau.



Tafuta detail zoote, timetable ya nacte.. Alafu tafuta direct call ya viongozi wa nacte wa juu.. Niwasiliane nao tuwaunguze hao wakuu wa vyuo.

Mheshmiwa ndalichako alishakemea hili suala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom