WAZIRI WA ELIMU- unayajua yanayofanyika CBE- DODOMA?

WAZIRI WA ELIMU- unayajua yanayofanyika CBE- DODOMA?

Edson Zephania

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2011
Posts
517
Reaction score
112
Kuna mtafaruku mkubwa ndani ya Chuo cha elimu ya biashara kampasi ya Dodoma.
Mwaka 2009 kuna baadhi ya wanafunz waliokuwa mwaka wa pili (Advanced diploma) ktk matokeo yao ya semister ya nne walipata dicso(discontinuity) lakin wakiwa ktk harakati za kukata rufaa na kufuata taratibu zote wakapata ushawishi toka kwa mkuu wa idara ya masomo ya jioni kua rufaa hizo wasingeweza kushinda, hivyo kuwasaidia tu ni kwamba angewaruhusu kuwaingiza ktk programu ya masomo ya jioni.

Hivyo wanafunz hao wapatao kumi wakakubaliana nae na kweli wakaingizwa ktk program ya masomo ya jioni (NIGHT COLLEGE) wakaanza kusoma toka december 2009 wakafanya tena mitihani ya mwaka wa 2 upya (semister ya III&IV) wakaingia mwaka wa 3 mwez June 2010 wakafanya mitihani ya semister ya V vizuri bila matatizo, wakaendelea kusoma semister ya VI ilipofika wakati wa mitihani mwezi wa 5 mwaka huu, hapo ndipo zilipoanza sarakasi, wengine wakaambiwa kuwa hawakuwa wanafunzi HALALI wakati huo wengne kati yao wakiruhusiwa kufanya mitihani.

Wakajaribu kumfata yule mkuu wa idara ya masomo ya jioni (ndiye aliye wafanyia usajiri) akasema file lipo kwa Accademic officer, wakienda huko wanaambiwa file lenu halionekani, mpaka leo hawajapata suluhsho wanahangaika tu mtaani.

Sasa nikajiuliza tangu mwaka 2009 wanalipa ada, wanapewa namba za kufanyia mitihani, matokeo yanatoka, iweje leo si wanafunz halali?, kwa nini wengine waliokuwa na the same issue waruhusiwe kufanya mitihan?. Serikali iwasaidie vijana hawa kupata haki yao.
 
haituhusu cbe ipo jirani na bunge mngemtafuta huyo waziri
 
msiseme juu juu tu. haituhusu huenda kuna mchezo hapo kati

ningependekeza mamlaka husika wafuatilie na wachunguze ukweli wa suali hili.

huenda kuna mchezo mbaya kwa pande zote mbili
 
Tunaomba kujua Jinsia zao hao wanafunzi na Jinsia za hao waalimu. Labda tunaweza kusema neno linaloweza kumsaidia waziri kutoa ufumbuzi. Maana tunajua Kiputiputi hayupo pale Yeye anashughulika na Shule yake inayoitwa ASEKI(Asei & Kiputiputi)Hii ni nje ya Mada Lakini Neno kuu ni TUNAOMBA KUJUA JINSIA ZA WALENGWA WOTE.
 
Hvi m2 akidisco c anatakiwa arudie mwaka wa kwanza au utaratibu wa huko cbe ukoje?
 
Matatizo ya kufuata njia za mkato, wakate rufaa kwenye chombo husika!
 
Tunaomba kujua Jinsia zao hao wanafunzi na Jinsia za hao waalimu. Labda tunaweza kusema neno linaloweza kumsaidia waziri kutoa ufumbuzi. Maana tunajua Kiputiputi hayupo pale Yeye anashughulika na Shule yake inayoitwa ASEKI(Asei & Kiputiputi)Hii ni nje ya Mada Lakini Neno kuu ni TUNAOMBA KUJUA JINSIA ZA WALENGWA WOTE.
Wakati wa mchezo wote huo KIPUTIPUTI alikuwa ndiye M/mkuu wa chuo na amestaaf mwaka jana Sept/oct. Well wanafunz hao jinsia ni mchanganyiko, nilio fanikiwa kuwafahamu ni wasichana 2 wanaume 6. Tatizo ni kwamba wao kwa wao wakuu wa idara wanatupiana mpira wanamlaumu Academic officer(madame), na hv sasa nasikia wameitwa kampas ya dar kwa ajili ya issue hiyo.
 
Hvi m2 akidisco c anatakiwa arudie mwaka wa kwanza au utaratibu wa huko cbe ukoje?
si kurudia yaan hutakiwi kuonekana darasani, chuoni kama mwanafunzi, lakini mhawa wakuu wa idara waliokaa wakawaruhusu kuendelea ndiyo matatizo yote hayo.
 
"DICO" manake park your things and dissappear! lakini unaweza kuruhusiwa baada ya muda fulani kuomba same kozi, au ukaanza kozi nyingine katika idara tofauti immediately! l
hata hivo nashindwa kuilaumu uongozi wa CBE, kwani inaonesha
madenti hao hawakujua/hawajui taratibu na miongozo ya chuo chao! hili tatizo linawezekana kuwa ni uzembe wao! lakini pia huyo mkuu wa Idara
naye alikosea so anapaswa kuwajibika!
poleni sana watoto wa kitanzania!

Hvi m2 akidisco c anatakiwa arudie mwaka wa kwanza au utaratibu wa huko cbe ukoje?
 
Practically wanafunzi hao hawakistahili kuendelea na masomo.Hapo kutahitajika ushahidi wa barua za aliyewaruhusu km wanazo. Na pia cha kufanya wadai ada yao waondoke haraka au waanze upya. Chuo kinatakiwa kumwadhibu huyo aliyewaruhusu ingawa wanafunzi hutumia shortcut na kuamini hawatajulikana.
 
hizo barua, registration number, namba za mitihani, forms za mahudhurio darasani, forms za kusign coursework zote wanazo pamoja na risiti za ada pia.
 
Back
Top Bottom