Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumza na viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Njombe, Septemba 20, 2024 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali mkoani humo amesema kuwa wakati nchi inapata uhuru hakukuwa na chuo kikuu hata kimoja lakini pia kuanza darasa la kwanza ilikuwa kazi.
"Lazima tukubali kuwa toka tupate uhuru kuna hatua kubwa imepigwa katika maendeleo ya nchi ambayo yanatuwezesha kupiga kifua na kujidai kwa hatua kubwa iliyopigwa," amesisitiza Prof.
Mkenda.
Mkenda amesisitiza wakati tunapata uhuru barabara zilikuwa za vumbi na kwa upande wa elimu miundombinu haikuwa ya kutosha na haikuwa ya kuridhisha lakini kwa sasa katika nchi nzima kuna miradi mbalimbali ya barabara, maji, afya na elimu inatekelezwa kwa kasi kubwa.
Aidha, amewataka Watanzania kutambua Serikali inaendelea na uboreshaji wa huduma za jamii na ndio maana katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita imewekeza kwa kiasi kikubwa katika miundombinu ya elimu, afya, barabara na maji.
Amesema "Hatuwezi kukataa kwamba hakuna changamoto, zipo na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano anaendelea kutuekekeza sisi Mawaziri wake kuendelea kuzitatua ili ifike wakati tuzimalize kabisa."
Njombe yajivunia kupata Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kinachojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambayo itakuwa Taasisi ya Kwanza ya Elimu ya Juu katika mkoa huo.
Akizungumza Septemba 20, 2024 mkoani Njombe wakati wa kuanza kwa ziara ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita, Mbunge wa Jimbo hilo, Deo Mwanyika amesema uamuzi wa ujenzi wa kampasi hiyo utakuwa mkombozi kwa Wananjombe katika kupata elimu ya Juu.
Aidha, ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu Wananjombe wameshuhudia uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu ambapo shule mpya za msingi saba, sekondari 12 na mabweni 107 yamejengwa.