Waziri wa Elimu zimulike school buses, Watoto wako hatarini kupata maambukizi

minyoo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2013
Posts
22,405
Reaction score
21,100
Baada ya mashule kufungwa kupisha corona ipite zile Gari za kubeba wanafunzi maarufu kama school nyingi zilipaki majumbani, lakini baada ya mashule kufunguliwa wamiliki wa mashule wameamua kutumia mabasi machache kubana matumizi matokeo yake ni watoto kubanana sana mpaka wengine kukaa chini kukwepa mkono wa Trafik

Kibaya zaidi watoto wa darasa la kwanza wasiojua kujikinga na barakoa hukalishwa chini kwenye Vumbi lakini wale wakubwa wa darasa la tano sita hukaa kwenye viti. Ni hatari kubwa watoto wadogo kuteswa kwani ni wepesi kupata maambukizi ya COVID-19

Kuna baadhi ya maofisa Elimu ni wamiliki wa mashule najua wakiona Uzi huu watalifanyia kazi haraka ingawa si kwa wepesi kutokana na Waziri wa Elimu kuwa busy na kampeni kusahau kuwa kuna maambukizi ya Corona kwenye school bus.

Bus.jpg
 
Kwenye school bus mtoto wa darasa la kwanza hana haki huburuzwa sana, wengi wanaugua mafua sasa baada ya kupata Vumbi la kukalishwa chini ya korido ya bus.
 
CCM inawategemea walimu kwenye kura lakini imesahau watoto wao wanaugua mafua kisa wanabanana sana kwenye school bus
 
Shule gani inafanya hivyo , Ndalichako anaongozwa na tumbo.
Tatizo kubwa lipo kwa hizo shule za international zenye nembo za ST, wanatoza nauli kwa wazazi lakini watoto wao wanenda kukalishwa chini wanapata mafua
 
CCM hili watalipuza kwa sababu CCM wanataka maambukizi yawe makubwa kama Brazil wapate kisingizio cha kuahirisha uchaguzi mkuu.
 
Mkuu mpeleke mwanao shule kama ni mdogo, usitegemee saaana school bus
 
Ni shule gani ya serikali ina school bus? Si mlishaambiwa serikali haina mpango wa kuingilia mikataba isiyoihusu? Hata suala la ada si mliambiwa wazazi na shule mmalizane wenyewe huko? Ukiona mazingira sio favorable kwa mwanao mpeleke shule ya serikali; understood?
 
Tatizo kubwa lipo kwa shule za St mary’s na kwa kuwa Serikali hairuhusiwi kuingilia mikataba isiyowahusu ndiyo watumie mwanya huo kuwabananisha watoto wadogo kwa wakubwa kwenye mabasi? Kumbe Tatizo ni Serikali kutoa uhuru watoto wafanyiwe chochote na wamiliki wa mashule, mda kumalizana na shule siyo Tatizo, sasa tabu ipo kwenye usafiri unahatarisha Afya za watoto.
 
... ndio hivyo Mkuu; tegemea hayo maswali na majibu.
 
Watoto wengi wanakohoa wameambukizana kwenye school bus
 
... ndio hivyo Mkuu; tegemea hayo maswali na majibu.
Nasikia CCM wanazitegemea shule na walimu wake ambao watakuwa ni wakala wa CCM siku za uchaguzi ni vigumu CCM na waziri kulikemea hili janga.
 
Kama zimepunguzwa ni hatari kubwa. Tangu zamani magari haya hayatoshi, vitoto vinabananishwa sana, vinaamshwa usiku wa manane. Na usidhani mabus haya ni mali ya shule, ni chache zenye mabus. Shule nyingi huingia mikataba ya kubeba wanafunzi na kuandika majina ya shule hizo kwenye mabus na hapo TRA wanapigwa chenga ya mwili.
 
Maambukizi ya vikohozi mafua na hata covid 19 yanaenda kuendelea humo kwenye mabasi hayo, kibaya zaidi wale watoto wadogo wa darasa la kwanza la pili ndiyo hukalishwa chini kwenye korido za school bus Dereva, kondakta hajavaa barakoa hajanawa mikono anawapanga kwa kuwashika mikono, hajajipaka vitakasa mikono akifika majumbani huwashika mikono watoto wadogo, Serikali wapo busy na kampeni waziri wa Elimu kawasahau watoto wadogo wanataabika kwenye school bus. Serikali ya kutetea wanyonge ipo wapi?
 
Serikali ya kutetea wanyonge mbona haitetea watoto wadogo kwenye school bus? au wanyonge ni machinga peke yake?
 
Baada ya mashule kufungwa kupisha corona ipite zile Gari za kubeba wanafunzi maarufu kama school nyingi zilipaki majumbani, lakini baada ya mashule kufunguliwa wamiliki wa mashule wameamua kutumia mabasi machache kubana matumizi matokeo yake ni watoto kubanana sana mpaka wengine kukaa chini kukwepa mkono wa Trafik

Kibaya zaidi watoto wa darasa la kwanza wasiojua kujikinga na barakoa hukalishwa chini kwenye Vumbi lakini wale wakubwa wa darasa la tano sita hukaa kwenye viti. Ni hatari kubwa watoto wadogo kuteswa kwani ni wepesi kupata maambukizi ya COVID-19

Kuna baadhi ya maofisa Elimu ni wamiliki wa mashule najua wakiona Uzi huu watalifanyia kazi haraka ingawa si kwa wepesi kutokana na Waziri wa Elimu kuwa busy na kampeni kusahau kuwa kuna maambukizi ya Corona kwenye school bus.

Wazazi wao wako wapi?
 
Wazazi wao wako wapi?
Wazazi wengi hawajui kwani kipindi watoto hurejea toka shule wao huwa kwenye kuwajibika hawafahamu kinachoendelea
 
Nasikia CCM wanazitegemea shule na walimu wake ambao watakuwa ni wakala wa CCM siku za uchaguzi ni vigumu CCM na waziri kulikemea hili janga.
SIASA mpaka hujui thread yako inazungumzia nini.
 
Back
Top Bottom