Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Fedha na Mipango, Juma Malik Akil, amebainisha kuwa Zanzibar inaendelea kupata manufaa makubwa na hadhi ya kipekee ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hasa katika uimarishaji wa uchumi wake. Akizungumza wakati akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Juni 18, 2026, kufuatia uwasilishaji wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027, Waziri Akil alifafanua jinsi ushirikiano huo unavyosaidia kurahisisha upatikanaji wa mitaji na mikopo.
Katika ufafanuzi wake, Waziri Akil aliweka wazi siri ambayo wengi hawakuijua kuhusu deni la ndani la Zanzibar, akieleza kuwa zaidi ya 50% ya mikopo hiyo inatoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Alisisitiza kuwa hatua hiyo inasababishwa na ukweli kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni mwanahisa (shareholder) halali ndani ya Benki Kuu, jambo linaloipa mamlaka na fursa ya kupata rasilimali hizo kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Aidha, Waziri huyo aliongeza kuwa Zanzibar inafaidika na mamlaka kamili ya nchi (soverignty) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mchakato mzima wa kupata mikopo mikubwa. Alihitimisha kwa kusema kuwa, mikopo hiyo inayopatikana kupitia mwavuli wa Muungano inalipwa na kusimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hali inayopunguza mzigo wa kifedha moja kwa moja kwa upande wa Zanzibar na kuimarisha utengamano wa kiuchumi.