Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Napendekeza matumizi ya TEHAMA kuwa chaguo namba 1 kwa shughuli za Serikali, mambo yote ya Kiserikali yatumie mifumo ya TEHAMA. Waziri wa Fedha amesema kuwa Matumizi ya TEHAMA yanawezekana na itaokoa gharama kubwa kwa serikali.
Amesema kuwa unakuta mtu anasafiri siku 3 au 4 kwenda kuhudhuria kikao cha masaa 3 au 4 anaacha kuhudumia wananchi wakati angeweza shiriki kikao hicho akiwa mahali popote, au mtu anakusanya kundi kubwa la watu kutoka sehemu mbalimbali na wakati mzungumzaji ni 1 tu mkutano huo ungweza kufanyika kwa kutumia TEHAMA na mambo yakawa sawa.
Amesema Serikali inajenga chuo cha TEHAMA na bado tunaogopa TEHAMA, amesisitiza kuwa matumizi ya TEHAMA hayaepukiki katika zama hizi.
Amesisitiza kuwa mbona Mahakama wameweza kutumia Tehama kwanini Serikali inaogopa TEHAMA?