Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 bungeni leo, ameeleza kuwa hali ya deni la serikali hadi kufikia mwezi Machi 2026 imefikia shilingi trilioni 114.34.
Katika kiasi hicho cha deni, Mhe. Balozi Khamis amebainisha kuwa deni la ndani linajumuisha shilingi trilioni 38.45 (sawa na asilimia 33.6), wakati deni la nje likiwa ni shilingi trilioni 75.89 (sawa na asilimia 66.4). Waziri amesisitiza kuwa deni hilo limeelekezwa katika maeneo ya kimkakati yanayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi, ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji, sekta ya nishati, pamoja na mifumo ya mawasiliano.
Akiwatoa hofu wabunge na wananchi, Waziri wa Fedha amesema kuwa tathmini iliyofanyika mwezi Novemba 2025 inaonesha kuwa deni la nchi bado ni himilivu kwa kipindi cha muda wa kati na mrefu. Amesema kuwa viashiria vyote vya deni viko chini ya ukomo wa kimataifa; kwa mfano, thamani ya sasa ya deni kwa pato la taifa ni asilimia 39.6 pekee ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55, jambo linalothibitisha kuwa nchi ina uwezo mkubwa wa kuhimili deni lake bila kutikisa misingi ya uchumi.