Waziri wa Fedha: Serikali iko mbioni kupendendekeza chanzo kipya cha mapato kupata fedha za Wizara ya ujenzi kutatua dharura

Waziri wa Fedha: Serikali iko mbioni kupendendekeza chanzo kipya cha mapato kupata fedha za Wizara ya ujenzi kutatua dharura

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni pendekezo la chanzo kipya cha mapato kitakachowezesha Wizara ya Ujenzi kupata fedha itakayotumika kusaidia masuala ya dharura.

Dkt. Mwigulu amesema hayo wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ambapo amesema chanzo hicho kitaanza kutumika kuanzia mwaka ujao wa fedha 2024/2025.

“Kuna uhitaji wa bajeti kwa ajili ya marekebisho ya barabara ambazo zimeharibika na tunalifanyia kazi hilo na hivi tunavyoongea tunatarajia tutakapokuja kwenye bajeti kuu tutatoa tamko kuhusu bajeti mahususi ya dharura kurejesha barabara zilizoharibika na tulivyokaa na wenzetu wa Wizara ya Ujenzi wametuamhia kwa upande wa ujenzi inahitajika takribani Tsh. bilioni 700 mpaka Tsh. trilioni 1”

“Kwa upande wa TARURA zinahitajika takribani Tsh. bilioni 300 na uwekezaji uliofanyika katika barabara hizi ni takribani Tsh. trilioni 40 na Serikali haiwezi ikaacha uwekezaji huu ukapotea hivihivi”

Akizungumzia uharibifu wa miundombinu ya barabara uliotokana na mvua za El-Nino zilizoharibu barabara pamoja na athari za kimbunga Hidaya amesema “Nilikuwa namuonea Huruma Waziri mwenzangu Bashungwa alikuwa akifika ‘site’ barabara imeharika Wananchi wamekwama anasema Waziri wa Fedha nimpelekee fedha lakini fedha hizo ambazo zinatakiwa zipatikane kimsingi sio za dharura tunalazimika tukate kutoka maeneo mengine na kwakuwa imekuwa ikijirudia itupe funzo kuwa tunahitaji tupate chanzo ambacho kitakuwa kikijilimbikiza wakati wa amani kiweze kutumika wakati wa dharura”

Pia soma:
 
Kicha Cha habari kinapotosha maelezo ya Waziri.

Ser

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni pendekezo la chanzo kipya cha mapato kitakachowezesha Wizara ya Ujenzi kupata fedha itakayotumika kusaidia masuala ya dharura.
Heading Yako inapotosha maelezo ya Waziri.

Waziri amesema wataleta Bajeti mahususi ya around 1Trln Ili kutatua ujaribu wa Barabara kutokana na mvua Kwa TanRoads na TARURA.

On top of that watapendekeza chanzo kipya Cha kupata Fedha za Bajeti ya Ujenzi wakati wa Hotuba Kuu.

Napendekeza betting ichangie pesa hizo.
 
Iko sahihi, sikiliza video utaelewa
 
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni pendekezo la chanzo kipya cha mapato kitakachowezesha Wizara ya Ujenzi kupata fedha itakayotumika kusaidia masuala ya dharura.
Chanzo kipya ni kupunguza matumizi ya wabunge, mishahara, idadi, Aina ya nishati wanayotumia mfano toka diesel kwenda gesi na serikalini hivyo.
 
Bongo unazaliwa mpaka unakata moto wewe ni kukamuliwa tu, labda ubahatishe uingie kwenye mrija.

Babu Talle anakula laki 2 kila akikaa ila na hali ya mtaani ilivo bado wanawaza kuwakamua wananchi. Tutafika tumechoka sana
 
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni pendekezo la chanzo kipya cha mapato kitakachowezesha Wizara ya Ujenzi kupata fedha itakayotumika kusaidia masuala ya dharura.
Huyu ameshindwa kuwa msaidizi mzuri wa Raisi, Kwani hatumibelimu yake ya uchumi kumshauri Raisi pamoja na Sirikali yote Kwa jumla
 
Hakuna hoja za kubana matumizi wao kila siku ni tozo?
Mtu anasafiri na boeing dreamliner na kikosi cha mamia ya watu, watueleze kila safari moja bajeti yake ni kiasi gani.

Wizi na matumizi ya hovyo ya pesa za wananchi pesa zikiisha wanarudi kuwakamua wananchi.

Inasikitisha.
 
Back
Top Bottom