Waziri wa Fedha: Serikali iko mbioni kupendendekeza chanzo kipya cha mapato kupata fedha za Wizara ya ujenzi kutatua dharura

Waziri wa Fedha: Serikali iko mbioni kupendendekeza chanzo kipya cha mapato kupata fedha za Wizara ya ujenzi kutatua dharura


Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni pendekezo la chanzo kipya cha mapato kitakachowezesha Wizara ya Ujenzi kupata fedha itakayotumika kusaidia masuala ya dharura.
Hawa ccm nilazima na sio ombi kutoka madarakani kama uchaguzi ukifanyika
 
Hakuna hoja za kubana matumizi wao kila siku ni tozo?
Mtu anasafiri na boeing dreamliner na kikosi cha mamia ya watu, watueleze kila safari moja bajeti yake ni kiasi gani.

Wizi na matumizi ya hovyo ya pesa za wananchi pesa zikiisha wanarudi kuwakamua wananchi.

Inasikitisha.
Nani alibana matumizi akafaulu kutatua shida? Kubana matumizi kama yapi?
 
Nimpe mchemba chanzo kingine cha mapato kila abiria anayeenda mikoani au kuja Dar kwa basi au private akatwe 1000 tzs .
 
Nchi hii, na hivi wanajua kama sisi WADANGANYIKA mapoyoyo ni wengi, wanajifanyia wajisikiavyo, mtu wa chini ndio hali inazidi kuwa tete.
 

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni pendekezo la chanzo kipya cha mapato kitakachowezesha Wizara ya Ujenzi kupata fedha itakayotumika kusaidia masuala ya dharura.

Dkt. Mwigulu amesema hayo wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ambapo amesema chanzo hicho kitaanza kutumika kuanzia mwaka ujao wa fedha 2024/2025.

“Kuna uhitaji wa bajeti kwa ajili ya marekebisho ya barabara ambazo zimeharibika na tunalifanyia kazi hilo na hivi tunavyoongea tunatarajia tutakapokuja kwenye bajeti kuu tutatoa tamko kuhusu bajeti mahususi ya dharura kurejesha barabara zilizoharibika na tulivyokaa na wenzetu wa Wizara ya Ujenzi wametuamhia kwa upande wa ujenzi inahitajika takribani Tsh. bilioni 700 mpaka Tsh. trilioni 1”

“Kwa upande wa TARURA zinahitajika takribani Tsh. bilioni 300 na uwekezaji uliofanyika katika barabara hizi ni takribani Tsh. trilioni 40 na Serikali haiwezi ikaacha uwekezaji huu ukapotea hivihivi”

Akizungumzia uharibifu wa miundombinu ya barabara uliotokana na mvua za El-Nino zilizoharibu barabara pamoja na athari za kimbunga Hidaya amesema “Nilikuwa namuonea Huruma Waziri mwenzangu Bashungwa alikuwa akifika ‘site’ barabara imeharika Wananchi wamekwama anasema Waziri wa Fedha nimpelekee fedha lakini fedha hizo ambazo zinatakiwa zipatikane kimsingi sio za dharura tunalazimika tukate kutoka maeneo mengine na kwakuwa imekuwa ikijirudia itupe funzo kuwa tunahitaji tupate chanzo ambacho kitakuwa kikijilimbikiza wakati wa amani kiweze kutumika wakati wa dharura”

Pia soma:
Mnafikiri itakuwa ni chanzo gani?

Si kwingine ni aidha kwenye line za Simu, miamala ya pesa za ki electroni, vinywaji hususani soda na pombe au kwenye nishati ya mafuta (petrol/diesel na umeme)

Akili na uwezo wa serikali ya CCM kwenye ishu ya mapato ni kwenye maeneo hayo tu ambayo basically ni huduma.

Na unapogusa sekta ya huduma (service oriented secto) kwa kuishambulia kwa kuiwekea tozo na Kodi lukuki, basi Moja kwa Moja ni kutaka kuyafanya maisha ya wananchi wa kawaida kuwa magumu zaidi na zaidi maana bei ya huduma hizo itapanda maradufu!
 
Back
Top Bottom