Waziri wa Fedha: Serikali iko mbioni kupendendekeza chanzo kipya cha mapato kupata fedha za Wizara ya ujenzi kutatua dharura


Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali iko mbioni kupeleka Bungeni pendekezo la chanzo kipya cha mapato kitakachowezesha Wizara ya Ujenzi kupata fedha itakayotumika kusaidia masuala ya dharura.
Hawa ccm nilazima na sio ombi kutoka madarakani kama uchaguzi ukifanyika
 
Nani alibana matumizi akafaulu kutatua shida? Kubana matumizi kama yapi?
 
Nimpe mchemba chanzo kingine cha mapato kila abiria anayeenda mikoani au kuja Dar kwa basi au private akatwe 1000 tzs .
 
Nchi hii, na hivi wanajua kama sisi WADANGANYIKA mapoyoyo ni wengi, wanajifanyia wajisikiavyo, mtu wa chini ndio hali inazidi kuwa tete.
 
Mnafikiri itakuwa ni chanzo gani?

Si kwingine ni aidha kwenye line za Simu, miamala ya pesa za ki electroni, vinywaji hususani soda na pombe au kwenye nishati ya mafuta (petrol/diesel na umeme)

Akili na uwezo wa serikali ya CCM kwenye ishu ya mapato ni kwenye maeneo hayo tu ambayo basically ni huduma.

Na unapogusa sekta ya huduma (service oriented secto) kwa kuishambulia kwa kuiwekea tozo na Kodi lukuki, basi Moja kwa Moja ni kutaka kuyafanya maisha ya wananchi wa kawaida kuwa magumu zaidi na zaidi maana bei ya huduma hizo itapanda maradufu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…