Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Waziri wa Habari, Mawasiliano, na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry William Silaa (Mb), ameteua Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa mujibu wa Sheria ya TTCL ya mwaka 2017, Kifungu cha 7(2)(3) kikisomwa pamoja na Kipengele cha 1(1) cha Jedwali la Sheria hiyo.
Uteuzi huu unahusisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali, walioteuliwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 26 Novemba 2024 hadi 25 Novemba 2027. Wajumbe walioteuliwa ni:
Soma Pia: Baada ya Wenyeviti kuondolewa, Waziri Jerry Silaa avunja Bodi za TTCL, Shirika la Posta (TPC) na UCSAF
- Bw. Onorius John Njole – Mwandishi Mkuu wa Sheria (CPD).
- Bw. Khalfan Salim – Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar.
- Bw. Mohammed Ame Makame – Mkurugenzi Mtendaji wa Zanzibar Civil Status Registration Agency (ZCSRA).
- Bw. Meshack Joram Anyingisye – Kamishna wa Bajeti, Wizara ya Fedha.
- Prof. Saudin Jacob Mwakaje – Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
- Bi. Kapwete Leah John – Meneja wa Huduma za Sheria, Bodi ya Utalii.