Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 339
- 678
Na Elius Ndabila
0768239284
Mh Japhet Ngayilonga Hasunga Waziri wa Kilimo, nianze kwa kukupongeza kwa kazi kubwa unazofanya hasa upande wa Wizara nyeti inayobeba maisha ya Watanzania zaidi ya milioni 55. Wizara ya kilimo ndiyo wizara mama ambayo inabeba karibia Wizara zote za kisekita.
Unapozungumzia wizara ya uvuvi. Wizara ya Viwanda, Wizara ya Fedha n.k zinategemea uimara wa Wizara yako ya Kilimo. Hivyo ninaweza kusema kuwa wizara ya kilimo ndiyo wizara inayobeba maisha ya nchi kwani inakadiliwa Watanzania asilimia 80 ni wakulima.
Siku chache zilizopita Mh Waziri ulinukuliwa ukisema watu wanaolalamikia juu ya ukubwa wa bei ya mahindi waende wakalime ya kwao. Ulisistizakuwa wakulima wanafanya kazi zote wao, kwa nini tuwapangie bei? Mimi nilikuelewa sana sana na kauli yako iliwapa matuaini makubwa wakulima wa Mahindi na mazao mengine kwa kuondoa mawazo potofu yaliyokuwa yanajengeka kuwa Waziri yuko busy na korosho na kusahau maeneo mengine. Kauli yako hiyo imejaribu ku clear all doubt. Kudos!
Leo Mh Rais Dk. Magufuli akiwa Morogoro amekazia tamko lako kuwa wakulima wa mahindi wasipangiwe bei. Amesema anayeona mazao ya chakula yanabei aende akalime kwani sasa ni msimu wa mvua. Na Rais ameenda mbali kwa kuipongeza mikoa iliyofanya vizuri mwaka jana ikiongozwa na mkoa wa Songwe, Rukwa na Katavi kuwa iliongoza kwa uzalishaji wa mazao.
Kauli ya Mh Rais inazidi kuwapa matumaini Watanzania wengi ambao walikuwa wanatumia nguvu zao nyingi kulima, lakini unapokuja kwenye swala la bei lilikuwa linakatisha tamaa. Na mara zote kauli ya Rais ni agizo na sheria. Katiba inampa mamlaka hii.
Mh Hasunga ninaomba nikurudishe nyuma kidogo hasa bada ya kusikia kauli ya Mh Rais ambayo bila shaka nchini kote wakulima wanashangilia hivi sasa. Mara nyingi nimekuwa nikiandika sana juu ya pareto lakini inawezekana ninayo andika hayakufikii kwa sababu ya uwingi wa kazi. Leo ninamini wasaidizi wako watakufikishia kwa kuwa nitawatag wote. Juu ya zao hili mhimu na ambalo linaweza kubadilisha maisha ya wakulima haraka lakini naona kama umekuwa hulitupii macho sana.
Kwa Watanzania ambao labda hamlijui zao hili la pareto linalimwa sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini hasa Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa. Ni zao ambalo likishaanza kutoa maua ambayo ndiyo huchumwa mkulima anashauriwa kuchuma kila baada ya siku 7 hadi 14. Maua haya inasemekana yanatumika kutengenezea sumu na mafuta ya ndege, chanzo ni PharmaTutor | Pharmacy Infopedia.
Changamoto ya hili zao ni kwamba bei zake hupangwa na mununuzi na mkulima hana uwezo wa kujipangia bei. Munnuzi ndiye hupanga bei na inasemekana bei yake kwa sasa ni zaidi ya 3300/= kwa kilo lakini mkulima hulipwa 2300/= na kuambiwa pesa nyingine atalipwa mara baada ya pareto kufika kiwandani na kupima kama ina sumu. Hapa yapo maswali mengi ya kujiuliza huko kiwandani kuna mwakilishi wa wakulima anayeenda kuthibitisha kama kuna sumu au haipo kwenye hiyo pareto?
Na wanajuaje kuwa mtu X pareto yake ina sumu na mtu Y haina sumu wakati gunia moja mnaweza mkaweka zaidi ya watu watano? Je wizara haioni kama sasa umefika muda mwafaka wa wakulima hawa kuangaliwa kwa jicho linguine? Kwa nini serikali isiruhusu wanunuzi wengine kununua pareto ili kuwe na ushindani kuliko sasa kuwaachia TPC tu ambao wanaweza kutumia huo mwanya kuwanyonya wananchi?
Na kwa nini vyombo vya kupimia sumu visiwekwe huko vijijini wanakonunulia hilo zao ili mkulima zao lake linapoondoka ajue anastahili kupewa hiyo 2300/= na aache kusubiria hii 1000/= inayokuja kama bahati nasibu?
Ushauri wangu kwako Mh Hasunga chukua hatua kuwaokoa wananchi ninamini Mh Rais atakuunga mkono. Ruhusuni wanunuzi wengi ili kuondoa urasimu huu ambao unakuwa unamkandamiza mkulima. Ninaamini mkiruhusu wanunuzi wengi kwanza pareto itapanda juu na serikali itajipatia fedha nyingi kutokana na kodi. Hii pia itaongeza tija kwenye uzalishaji na wananchi kujiletea maendeleo.
Ninadhani kuna haja kubwa serikali kupitisha macho kwenye zao hili kama ilivyo kwenye korosho. Nchi ili kuingia kwenye uchumi wa kati unahitaji kilimo na viwanda, lakini hakuna viwanda bila kilimo. Baada ya kumaliza korosho na Pareto tuingie kuhamasisha watu kulima sana Iliki/CARDAMOM kwani ni moja ya zao ambalo linatafutwa sana Duniani. Na inasemekana nchi kama za Syria na Nepal wanapenda sana Iliki ya Tanzania.