Waziri wa Maji ingilia kati DAWASA, hali ya maji Dar ni mbaya sana

Waziri wa Maji ingilia kati DAWASA, hali ya maji Dar ni mbaya sana

LUS0MYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2011
Posts
866
Reaction score
1,109
Mheshimiwa Waziri wa Maji matatizo ya maji ya miaka kumi iliyopita yamerudi katika jiji la Dar es Salaam pamoja na kwamba hakuna taarifa ya kupungua kwa maji.

Hali ni mbaya zaidi kwa DAWASA Kimara ambapo pamoja na kupitiwa jirani na bomba kubwa kutoka Ruvu juu uhakika wa maji ni mdogo.

Hali ya utendaji imeshuka sana na upotevu wa maji unaonekana mabarabarani. Watumishi wasio waaminifu wanashirikiana na magari ya wauza maji ambayo mengi yanamilikiwa kwa siri na watu wa DAWASA.

Huduma kwa wateja imekuwa mbovu na hata mwitikio wao umekuwa mbovu. Mafundi wanaopita mtaani hawana sare wala vitambulisho hivyo inakuwa vigumu kuwatofautisha na vishoka.
 
Kwanini walimtoa yule muhandisi LUHENEJA sijui kama nimepatia pale DAWASCO na kumpeleka kazi na ajira sasa kwa VC ambako kimsingi hakuna kazi zenye madhara ya moja kwq moja kwa watu?
 
Ukonga banana ni miezi minne sasa ukiwauliza dawasa kinyerezi shida nini hakuna jibu la maana.
 
Tukikaa utasikia tutazalisha umeme mpaka tuwauzie Wakenya wakati shida ndogo ndogo zetu tu bado hatujatatua tunataka sifa za Nje...Nchi bado inasumbuka na maji 2024 na vyanzo vya maji vipo vya kutosha...
 
Afadhali huko angalau yanatoka mara Moja Kwa miezi minne.kule msakuzi,chama,mpiji magoe,makabe,machimbo hakuna kabisa huduma ya maji.yaani hawajaungwa na hiyo huduma.Ni mwendo wa kuletewa maji machafu ya chumvi na magari.Halafu kunawapuuzi wanasema mama anafanya kazi nzuri.upuuzi kabisa
 
Back
Top Bottom