Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amewataka watumishi wa Wizara ya Maji kukagua na kujiridhisha na thamani ya fedha katika miradi

Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amewataka watumishi wa Wizara ya Maji kukagua na kujiridhisha na thamani ya fedha katika miradi

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
AWESO AHITIMISHA VIKAO VYA IDARA KWA IDARA WIZARA YA MAJI, ASEMA TAASISI ZINAFUATA
IMG-20240614-WA0006.jpg

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akihitimisha Wiki ya Vikao vya Idara kwa Idara amewataka watumishi wa Wizara ya Maji kukagua na kujiridhisha na thamani ya fedha katika miradi maji ili kuisaidia wizara kutimiza azma ya Rais wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kufikisha huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini kwa asilimia 85 na mijini asilimia 95 .

Amesema hayo leo tarehe 13 Juni, 2024 katika ofisi za Wizara, Mtumba jijini Dodoma wakati wa kikao kazi na watumishi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini , pamoja na Kitengo cha Ukaguzi na amewataka wataalamu wote katika vitengo hivyo kuwa sehemu muhumu ya wizara ili kuepuka changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi.

Waziri Aweso amehitimisha wiki ya vikao kazi vya Idara kwa Idara kwa watumishi na watendaji wa Wizara ya Maji akitoa wito kwa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maji kujipanga kwani zitafuata.

Lengo la vikao kazi hivi ni kuongeza ufanisi katika utendaji wa sekta ya Maji na kutoa dira ya mageuzi ya ufanyaji kazi kwa watendaji.
IMG-20240614-WA0007.jpg
IMG-20240614-WA0009.jpg
IMG-20240614-WA0010.jpg
IMG-20240614-WA0011.jpg
IMG-20240614-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom