Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Waziri wa Sheria wa Malawi amesafiri kwenda Geneva nchini Uswizi kuhudhuria Mkutano wa 46 wa Baraza la Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Mkutano uliofanyia kwa njia ya kidigitali, na kuhutubia ukumbi uliojaa viti bila kuwepo mtu yeyote!
Mitandao ya kijamii imemshambulia Titus Mvalo kuwa tamaa yake ya kutaka pesa za marupurupu ya vikao imempeleka ughaibuni kwenye mkutano ambao alipaswa kuhudhuria kwa njia ya mtandao.
Washiriki wengine wote walikuwa katika nchi zao wakitumia njia za kidigitali kama Mikutano ya Zoom kufanikisha kuhudhuria kikao hicho.
Lakini Waziri huyo wa Malawi alisafiri hadi Geneva kuzungumza na washiriki anaowaona kwa njia ya video pekee.
Akizungumza kutoka katika ukumbi wenye viti 1490 lakini usio na watu mjini Geneva, Waziri Mvalo amesema nchi yake ni mfuasi mkubwa wa ushirikiano wa kimataifa, na ikiwa kama mwanachama wa Baraza la Haki za Binadamu itakuwa mfano wa kusimamia haki za binadamu.
"Nchi zote, kubwa na ndogo, zenye nguvu na zisizo na nguvu zinapaswa kufurahia haki sawa, na tunataka kuutengenea Umoja wa Mataifa tunaoutaka," Waziri Mvalo alisema.
Hata hivyo, serikali ya Malawi imesisitiza kuwa mkutano wa mwaka huu ulitakiwa kufanyika kwa njia zote, yaani njia ya kidigitali na ana kwa ana, na kuwa ilikuwa ni muhimu kwa Waziri huyo kusafiri kuhudhuria mkutano huo kutokana na umuhimu wake kwa Malawi.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa huu ulikuwa Mkutano wa kwanza kwa Malawi, hivyo ni muhimu kwa Waziri Mvalo kukutana na viongozi wa juu wa Baraza hilo ili kuweka sawa mazingira ya utendaji kazi wa taifa lake.
Mkutano wa 46 wa Baraza la Haki la Umoja wa Mataifa unafanyika kuanzia Februari 22 hadi Machi 23 mwaka huu. Baraza hilo linaundwa na nchi 47, likiwa na lengo la kuimarisha, kutetea na kusimamia haki za binadamu duniani. Miongoni mwa ajenda zitakazozungumzwa katika mkutano wa mwaka huu ni pamoja na athari za maambukizi ya virusi vya corona kwa haki za binadamu.
Chanzo: Malawi Talk