Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 525
- 2,950
ANADANGANYA kusema kwamba tatizo ni Sheria ya Bunge ,kwamba yeye hawezi ifuta.
Tatizo wala sio Sheria ya usalama Barabarani ,Sheria ipo wazi kabisa,Sheria ya usalama Barabarani (Road Traffic Act ) Sura No.168 toleo la 2023 kifungu cha 31(1) kinasema hivi ,
" For the purpose of ensuring compliance with the provision of this act and conditions attached to a driving licence, every licence shall have a number of points which may be deducted proportionally whenever a driving licence holder commits or is convicted of an offence under this Act ".
Sheria ipo too general , hakuna sehemu Sheria imesema idadi ya pointi kwenye leseni ,wala haijataja muda wa kufungiwa ,wala haijataja orodha ya adhabu na makosa,Wala Sheria haijataja taratibu za namna utaratibu huu wa Penalty Licence Point System utatekelezwa ,Sheria imetoa nafasi kwa Waziri kutengeneza kanuni (Regulations/Subsidiary legislations) za namna mfumo huu uta-operate.
Kifungu cha 31(2) cha Sheria ya usalama Barabarani (Road traffic Act) kinasema "The Minister may make regulations prescribing the manner in which the driving licence point System shall operate"
Kwahiyo,hadi hapo tatizo sio Sheria,tatizo ni kanuni zilizotungwa na kufanyiwa marekebisho na Wizara ya mambo ya ndani kupitia waziri na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali namba 420 tarehe 11/7/2025: na kuitwa "The Road Traffic,Drivers licence point System:Amendment Regulations of 2025".
Kanuni ndio zimeweka idadi ya makosa 35 ikaweka pia makosa ya mmiliki wa chombo kubebeshwa Dereva,kanuni ndio zimeweka idadi ya Pointi 15 kwa kila leseni ambazo ni chache,kanuni ndio imeweka adhabu ya leseni kufungiwa miezi 6 mara ya kwanza,miezi 12 mara ya pili,miezi 36 mara ya tatu,miezi 76 mara ya nne pamoja na kufutiwa madaraja na kuanza upya Daraja la mwanzo kabisa.
Kanuni zimemfanya trafiki kuwa msimamizi mkuu wa huu mfumo badala ya kutumia kamera na mifumo ya kidigitali ,kanuni hazijaweka utaratibu wa kukata Rufaa,kanuni hazijaweka utaratibu wa kumpa Pointi Dereva akiendesha vizuri kwa muda fulani kama motisha,ni kanuni ndio zimeweka utaratibu wa kukatwa pointi bila kikomo kwa safari moja.Serikali imetunga hizi kanuni kukomesha madereva kwa adhabu kali bila kujali tatizo la miundombinu yetu,uadilifu wa trafiki barabarani na mambo mengine.
Tatizo hata sio sheria katika huu utaratibu wa mfumo wa adhabu ya alama (Demerit/Penalty Point System) sababu sheria
imeelezea kwa ujumla ,tatizo ni kanuni zinazoelezea utekelezaji wa sheria ndio zinachangamoto
wa namna ya utekelezaji.Nchi nyingi duniani na Afrika kama
Uingereza,Marekani,Ufaransa,Italia,Ujerumani ,Canada,Uganda,Kenya,Zambia,Ghana,Zimbabwe,Afrika
ya kusini ,Rwanda na nchi nyingine wana huu mfumo wa adhabu ya alama (Demerit/Penalty Point System).Hivyo sio jambo geni
Ila hizi nchi na nyingine namna mfumo huu wa pointi unavyotekelezwa sio kwa lengo la
kuwakomesha madereva na wadau wa usafirishaji kama sisi Tanzania bali kwa lengo la kupunguza ajali,kuongeza
nidhamu na umakini kwa madereva,kulazimisha madereva kufuata na kuheshimu sheria za
barabarani bila kuwaumiza madereva.
Ila kwetu Tanzania namna mfumo wa adhabu ya alama zilivyo katika
utekelezaji wake kupitia kanuni ni kama tumedhamiria kuumiza na kufukarsha madereva,kuwaongezea madereva msongo wa mawazo,kuongeza rushwa barabarani,kuongeza
ajali barabarani badala ya kupunguza,kupunguza idadi kubwa ya madereva katika mzunguko wa
nguvu kazi, kuvuruga tasnia ya usafirishaji nchini (Logistic Industry),kuongeza gharama kubwa
katika uendeshaji wa biashara ya usafirishaji sababu ya uhaba wa madereva kulingana athari ya kanuni hizi na kufukarisha madereva kutokana na kutofanya kazi sababu ya kufungiwa leseni ,kuongeza mgogoro kati ya madereva wa vyombo vya moto na askari wa usalama
bararani.
Mfano ,tatizo la KIWANGO cha Rushwa Barabarani kimejidhihirisha katika kipindi hiki cha majaribio ya mfumo huu kwani kiwango cha Rushwa kimeongezeka sana Barabarani , madereva wakikwepa wasipunguziwe pointi na matrafiki wakidai rushwa ili wasikate pointi kupitia faini kwenye POS.
Binafsi kwa nafasi yangu ,mbali na kuwasiliana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mh.Patrobas Katambi tarehe 16/Septemba /2026 kumueleza changamoto ya suala hili.Pia nimeandika mapendekezo yangu yenye kurasa 7 na nimewasilisha kwa Waziri wa mambo ya ndani Mh.Patrobas Katambi kuhusu suala hili.
Serikali kupitia Wizara ya mambo ya ndani na Waziri wa mambo ya ndani futeni hizi kanuni,shirikisheni wadau kuunda kanuni Mpya bora na nzuri kwa kuzingatia changamoto ya miundombinu yetu, ukosefu uadilifu kwa baadhi ya trafiki wetu ,hiii ni kwa ustawi wa pande zote Madereva,wadau wa usafirishaji,wananchi na Serikali kwa ujumla.
Abdul Omary Nondo.
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana Taifa -ACT Wazalendo.
30/Septemba/2026.