JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amezungumzia kukamatwa kwa watuhumiwa mbalimbali wa sakata la utekaji ambalo limekuwa likizungumziwa na vyombo mbalimbali vya habari katika siku za hivi karibuni huku likiacha taharuki kwa wananchi huku pia suala la kuteswa likitajwa kushamiri…….
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kitabu kilichoandikwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania,Dkt. Abubakari Zubeir kinachoitwa Mmomonyoko wa Maadili Nani Alaumiwe,Waziri Masauni ametaja takribani kesi nane na hatua zilizochukuliwa na serikali juu ya matukio hayo ya utekaji ikiwemo tukio la mtoto Albino aliyetekwa na kukutwa ameuawa na kunyofolewa viungo vya mwili,tukio la hivi karibuni la Edgar Mwakabela anayejulikana zaidi kwa jina la Sativa.
============
Gazeti la Mwananchi la Julai 2, 2024 likiwa na kichwa cha habari kikubwa kuhusu utekaji.