Je ni yule yule Membe aliyekuja na hoja ua OIC ? Leo kaja na habari za Wapemba ? Hivi hao wapemba wako wangapi ? Je kubeba mabango na kutoa ujumbe ni kuharibu ziara ya mkubwa ? Haki ya kupeleka ujumbe mbona inakataliwa ?
Ni ubabe na kumalizika na kufikia mwisho wa upeo wa utawala wa CCM kufikiri ,mambo ambayo yanahitajiwa kusemwa na wengine wanajipachika wengine ,ndio maana kila wanapojaribu wanaumbuka,si umeona mwengine , Mkuu wa Nchi Mheshimiwa Jemedari Mkuu wa Majeshi ya Tanzania anakuja na kali ya mwaka ,wananchi wapige kura kuwafichua wauaji maalbino,wanaooua vizere sijui majambazi na mambu kibao ,hivi hawa waliogunduliwa mpaka leo wamewafanya nini ?
Yule jamaa kakamwatwa na mabilioni kibao mpka leo Tanzania haijasema lolote na ushahidi kuwa mali aliyokuwa nayo hakuiwakilisha kakule alikohitajiwa kuzieleza ,amefanywa nini ? Mbona nasikia amepewa kamati aongoze ninachokuwa na wasiwasi hapa ni kuwa hii nchi wanataka kuwafanya wananchi wote ni wajinga ,hakuna jingine ,wanatuona akili zetu ziko chini zaidi ya wao ,jamani akili nywele kila mtu ana zake ,msitake kuwafanya wengine wafanane na ninyi kwa kuwaunga mkono mengine hayaungiki.
Nilijitahidi kumsifu huyu Mkuu wa Nchi na kuona timepata kiongozi kumbe tumepatikana.
Kura yangu sijawahi kuipeleka CCM na ndio kwa mambo haya hawaioni kabisa na wala hawana la kunishawishi.
Upinzani Tanzania tunahitaji Katiba mpya na tume mpya ya uchaguzi ,hakuna cha kungojea ,au maneno ya kila siku ya kusema hii katiba haina kasoro si ya kweli ni kutulazimisha kuwa na kifaa kilichochaa ambacho hakiwezi kutuvukisha kule tunakotaka kuenda.
Siku nikisikia CCM imeanguka katika kuiongoza Tanzania ndio siku nitakayokwenda kukata kadi ya CCM ili niendelee kuwa mpinzani.