Waziri wa Mambo ya Nje, Thabit Kombo akutana na Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje, Thabit Kombo akutana na Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29, 2025

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
WAZIRI WA MAMBO YA NJE AKUTANA NA TUME YA UCHUNGUZI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam, Februari 17, 2026.

Mkutano huo ambao umefanyika katika ukumbi wa Tanganyika uliopo jengo la Benki Kuu ya Tanzanja (BOT) jijini hapa, ni sehemu ya juhudi za Tume hiyo kukusanya taarifa, maoni na ushauri kutoka kwa viongozi mbalimbali.

Pamoja na mambo mengine, hoja zilizojadiliwa katika mkutano huo zilihusu maeneo ya tathmini ya athari za matukio hayo ndani ya nchi na kimataifa na ushauri wa hatua za kijamii na kisheria zinazochukuliwa ili kuimarisha amani, mshikamano wa kitaifa na kimataifa.

Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali ikiwemo waathirika wa matukio ya uvunjifu wa amani, kwa lengo la kukusanya ushahidi na taarifa zitakazoiwezesha kuandaa ripoti ya kina.

IMG-20260217-WA0082.jpg
IMG-20260217-WA0080.jpg
IMG-20260217-WA0079.jpg
IMG-20260217-WA0081.jpg
IMG-20260217-WA0083.jpg
 
Huku ndiyo tunaita kujitekenya na kucheka mwenyewe. Tume ambayo hata machinga anaweza kuitwa akakataa kwenda haina uhalali wowote.
 
Juzi alikutana na ICC leo na Tume ya Chande.
Nadhani kinachoendelea ni kuoanisha taarifa itokanayo na maswali ya ICC ili ioan nae kitackacholetwa na Tume.
 
Namuona mzee wangu jaji chande hapo 😄

Ova
 
Huyu kombo mtoto wa shehe Thabit Kombo ukimuangalia haraka utadhani sura ni kama wale watoto mahitaji yaani [ special needs.]
Zamani tuliita mataahira
 
Back
Top Bottom