Waziri wa Mambo ya Nje wa EU kutembelea Tanzania kujadili hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi

Kurunzi

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
10,198
Reaction score
11,630
Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya (EU) anawasili kesho jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo muhimu na serikali ya Tanzania kuhusu demokrasia, haki za binadamu na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Ziara hiyo ya siku tatu (Julai 8-10) inafanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus, Dkt. Constantinos Kombos, kwa niaba ya Mwakilishi Mkuu wa EU kwa Masuala ya Kigeni na Sera za Usalama, Kaja Kallas, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya.

Dkt. Kombos atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Thabit Kombo, kuhusu uhusiano wa EU na Tanzania, utawala wa kidemokrasia na ushirikiano wa kiuchumi chini ya mkakati wa Global Gateway, kwa mujibu wa taarifa ya EU leo.

🔹 Masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na:
  • Hali ya sasa ya kisiasa nchini Tanzania
  • Uchaguzi Mkuu wa 2025
  • Usalama wa kikanda, hususan katika eneo la Maziwa Makuu
Katika ziara hiyo, Dkt. Kombos pia atakutana na viongozi wa mashirika ya kiraia, wafanyabiashara, na wadau wengine muhimu.

Waziri Thabit Kombo alitembelea makao makuu ya EU Brussels mnamo Aprili na kukutana na Kaja Kallas, Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa Koen Doens, na Makamu wa Rais wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) Thomas Östros ili kuimarisha mazungumzo ya kisiasa, uwekezaji na maendeleo endelevu.

📌 Muktadha wa ZiaraKatika mwezi Mei, Bunge la Ulaya lilipitisha azimio kali kulaani mashtaka ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu, likieleza wasiwasi mkubwa juu ya mashitaka yenye nia ya kisiasa ambayo yanaweza kumhukumu kifo.

Bunge hilo lilitaka:
  • CHADEMA iruhusiwe kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Oktoba 2025
  • Serikali ya Tanzania ifanye mazungumzo ya kisiasa na vyama vyote kuhusu mabadiliko ya sheria za uchaguzi
  • Kuheshimiwa kwa haki za vyama vya siasa
  • Uchaguzi uwe huru na wa haki

Azimio hilo pia lililaani ukandamizaji wa kisiasa, kukamatwa kiholela, na usumbufu dhidi ya wanasiasa wa upinzani na watetezi wa haki za binadamu.
Wabunge wa Ulaya walitaka:
  • Adhabu ya kifo ifutwe Tanzania na hukumu zote zibadilishwe
  • Ushirikiano wa maendeleo wa EU na Tanzania, hasa chini ya mpango wa Global Gateway, uendane na haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na viwango vya haki katika mfumo wa sheria.

🇪🇺 Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa wafadhili wakubwa wa misaada ya maendeleo kwa Tanzania katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kupitia mkakati wa Global Gateway (2021–2027), EU imetenga euro milioni 990 (zaidi ya TZS trilioni 3) kusaidia sekta ya nishati na maeneo mengine muhimu nchini Tanzania.
 
While we are in meeting hatunaga mbaya, kila kitu kitakuwa sawa
 
Mara ooh wapige ban…. Mara oooh thr Hague

Hao jamaa wana interests zao na as long as natural resources zetu wanazila…. They become quiet
 
Waziri wa Mambo ya Nje wa EU kutembelea Tanzania kujadili hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi

📍 Julai 7, 2025
✍️ Na Mwandishi wa TBI, Dar es Salaam

Two Kombos in the meeting.
 
Mara ooh wapige ban…. Mara oooh thr Hague

Hao jamaa wana interests zao na as long as natural resources zetu wanazila…. They become quiet
Ni Bora iwe hivyo kuliko hili likibaraka kuchukua nchi
 
MKUTANO HUO BILA KU ENGAGE CHADEMA NI KUJA KULA PER DIEM
 
Kumuweka ndani mwenyekiti na kuzuia Chadema kufanya shughuli za kisiasa ni hatua za kiduanzi zilizochukuliwa na serikali inayoogopa uchaguzi huru na haki.
toa kende zako humu acheni ujinga
 
Mara ooh wapige ban…. Mara oooh thr Hague

Hao jamaa wana interests zao na as long as natural resources zetu wanazila…. They become quiet

Sasa wewe kweli kwa akili yako tu ya kawaida, CCM wanalinda mali zetu na chini ya CCM hazijaliwa.....!!?
 
Cypriot Foreign Minister Will Visit Tanzania, Talk EU Investments​

July 6, 2025

By The National Herald

Cyprus’ Foreign Minister Constantinos Kombos, will visit Tanzania from 8 to 10 July on behalf of the European Union’s (EU) High Representative for Foreign Affairs and Security Policy Kaja Kallas, to reinforce the bloc’s relationship.

Kombos will meet with Tanzania’s Minister for Foreign Affairs and East African Cooperation, Hon. Mahmoud Thabit Kombo, as well as members of civil society, business leaders, and other key stakeholders to discuss EU–Tanzania relations, the upcoming 2025 General Elections, economic cooperation under the Global Gateway strategy, and regional security developments, notably in the Great Lakes region.

“Tanzania is a trusted and stable partner in a strategically important region. As we celebrate 50 years of EU-Tanzania relations this year, the EU is committed to scaling up our cooperation – from investing in critical raw materials and digital transformation to supporting democratic values and inclusive growth. Together, we can unlock new opportunities that benefit both Tanzanian citizens and European partners,” said Kombos.

EU Ambassador to Tanzania and the East African Community, Christine Grau, said that “This visit underscores the EU’s commitment to a mature and strategic partnership with Tanzania, based on mutual interests.”

This follows Tanzania’s Minister Mahmoud Thabit Kombo’s April 2025 meetings in Brussels with Kallas, Director General for International Partnerships Koen Doens, and European Investment Bank (EIB) Vice President Thomas Östros to advance political dialogue, investment, and sustainable development.
 
Mh. Constantinos Kombos waziri wa mambo ya nje wa nchi ya Cyprus

View: https://m.youtube.com/watch?v=1grjC6yOyKk
Gwiji la diplomasia anayetumiwa na Umoja wa Ulaya EU kushawishi kuwaleta mezani pande hasimu Ukraine / Russia, Gaza, Syria n.k akiongea kuhusu juhudi hizo ... na sasa katumwa kuja Tanzania kujaribu kuongea na utawala (regime) ya rais Samia Hassan kuhusu R4 Maridhiano kuelekea 2025 na masuala mtambuka ya R4 yanavyoshawishi kuvutia uwekezaji, mahusiano kimataifa, misaada ya maendeleo n.k
 
Mara ooh wapige ban…. Mara oooh thr Hague

Hao jamaa wana interests zao na as long as natural resources zetu wanazila…. They become quiet
Unajidanganya sana.Yawezekana kwenye interests ulitaka kuandika tolerance ukasahau neno linaandikwaje.Wanataka baadaye msiseme hamkutusikilizwa na kupewa muda wa kutosha.
 
Haya amesemaje huyo mzungu wenu??
 
Back
Top Bottom