Doctor Mama Amon
Platinum Member
- Mar 30, 2018
- 2,311
- 3,513
Waziri wa Mazingira, Mhe. Masauni
Mheshimiwa Masauni,
Waziri wa Mazingira,
Uchafu ni kitu chochote kilicho kwenye nafasi isiyo yake.
Mfano, uchafu wa kimazingira unaojulikana kama "kelele" ni changamoto kubwa katika maeneo ya mijini.
Uchafu wa aina hii ni chanzo cha ukosefu wa usingizi, uziwi, msongo wa mawazo na kushuka kwa uzalishaji wenye tija mahali pa kazi.
Kwa mfano, ukiwa unafanya ka,i katika ofisi za Mkoa za NSSF Ilala muda wa saa saba mchana lazima usitishe kutoa huduma mpaka tangazo la vipaza sauti vya Msikiti ulioko pale la kuwaita waislamu waje kwenye swala limalizike.
Ni vivyo hivyo ukiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Upanga. Hapa pia ni kutokana na kelele za Msikiti wa Tambaza ulioko Barabara ya Umoja wa Mataifa.
Msikiti huu uko meta 100 kutoka Msikiti wa Wabuda, ulioko Mtaa wa Mindu.
Kule Kinondoni Kata ya Bunju, eneo la Mianzini, kuna msikiti umejengwa katikati ya makazi ya watu.
Katika eneo hili kero za vipaza sauti kwa jamii isiyo ya Waislamu ni endelevu, mpaka unajiuliza nani aliruhusu msikiti kujengwa katikati ya makazi ya watu?
Lakini sio hivyo tu. Upande wa pili wa Mianzini Bar kuna mchungaji mmoja saa 12 alfajiri kila Jumapili anafungulia spika yake mpaka mwisho. Kama una mgonjwa wa moyo lazima skate roho kwa sababu ya mtikisiko wa moyo.
View: https://youtu.be/TuPIDIsDWl0
Lakini, kuna uchafu wa kimazingira wa aina ya pili. Yaani watu kukusanyika kwenye eneo wasikopaswa kukusanyika.
Mfano, ukiwa Dodoma Mji Mpya eneo la Mwanga Bar, kila siku ya Ijumaa saa saba barabara inafungwa kwa ajili ya ibada ya Kiislamu inayofanyika barabarani mkabala na Baa hiyo.
Hali kama hii ni endelevu Kariakoo mkoani Dar es Salaam. Wote huu ni "uchafu" wa kumazingira barabarani.
Hii ni mifano michache tu, kwa ajili ya kufafanua ukubwa wa tatizo ninaloliongelea.
Na hii maana yake ni kwamba ama Waziri wa Mazingira hatekelezi wajibu wake ipasavyo au tunazo sheria na Kanuni zenye matobo yanayopaswa kuzibwa haraka ili kujenga jamii iliyo huru dhidi ya janga la kelele.
Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Tanzania ya mwaka 2004 pamoja na Kanuni zake za 2015 vinatambua "kelele" kama aina ya uchafuzi wa mazingira unaokatazwa kisheria kwa kutumia vigezo bayana.
Nimeambiwa na mtumishi mmoja wa NEMC Makao Makuu kwamba kifaa cha kupimia ukubwa wa kelele kinaitwa SOUND METER ambacho kinatumia kizio cha decibel (dB).
Lakini informer wangu huyu amesema hajui kifaa hiki kinapatikana dukani gani nchini Tanzania.
Hii maana yake ni kwamba hata wazalishaji wa kelele hawana uwezo wa kupata kifaa hicho kwa ajili ya kujifanyia self-monitoring, self-evaliation na self-control.
Lakini, kama tatizo ni upatikanaji wa tekinolojia ya kudhibiti kelele basi hiyo maana yake ni kwamba kuna matobo ya kisheria na kikanuni katika sheria zetu.
Tumetunga sheria ambazo hazitekelezeki. Na katika mazingira haya jawabu ni Tanzania kufuata nyayo za Rwanda.
Yaani kupiga marufuku vipaza sauti vinavyofungwa nje ya nyumba za ibada kama vile Makanisa na Masikiti.
Mwaka 2018 serikali ya Rwanda ilipiga marufuku misikiti kutumia vipaza sauri kwa ajili ya kuita watu kwenda kwenye sala (adhana).
Sababu iliyotajwa ni "uchafuzi wa mazingira kwa njia ya sauti." Hatua kama hizi zimechukuliwa kwa makanisa yapatayo 700 kwa sababu ya kelele zenye usunbufu kwa jamii.
Hatua za serikali ya Rwanda ni sehemu ya Dira ya Jiji la Kigali ifikapo mwaka 2040. Wanataka Jiji tulivu, linalovutia watalii na wawekezaji watakaokuwa huru dhidi ya kelele.
Wakati wa kujikosoa ni sasa.
Spika za kuita waumini