Waziri wa Michezo Mchengerwa unataka Simba SC na Yanga SC ziwe na umoja wakati wewe leo umeshindwa kuziunganisha!

Waziri wa Michezo Mchengerwa unataka Simba SC na Yanga SC ziwe na umoja wakati wewe leo umeshindwa kuziunganisha!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Halafu wenye akili kubwa kukuzidi akina GENTAMYCINE tukikusema kuwa wewe ni mzigo na hasara katika hiyo wizara utaona tunakuchukia au kukuonea wivu.

Leo ulipokuwa katika hafla ya kuwopongeza Tembo Warriors ulitaka vilabu vya Simba na Yanga viwe na umoja huku pia ukiitaka TFF nayo iviweke pamoja hivi vilabu.

Sasa kama wewe ni Waziri wa Michezo tena mwakilishi wa Kisera wa Serikali umeshindwa kuonyesha huo mfano leo ambapo wizara yako katika hafla hiyo iliamua kuwaalika viongozi waandamizi wa Yanga SC akiwemo Rais Injinia Hersi Said na kutowaalika viongozi waandamizi wa Simba SC unategemea ulilolihubiri kufanikiwa?

Na wafuatiliaji wa mambo mtambuka (masuala) akina GENTAMYCINE tunajua kuwa moja ya sababu kuu ya wewe kwa makusudi na unafiki wako utokanao na u Yanga wako uliwaalika viongozi waandamizi wa Yanga SC kwa kuwa Kocha Mkuu wa Tembo Warriors Salvatory Edward Mtaalam na Kocha wa Makipa wa Tembo Warriors.

Hivyo Mapunda ni wana Yanga SC wenzako na wenzenu na ndiyo maana hata 90% ya maudhui yako leo yalikuwa na hasira na povu kwa TFF huku ukifumba zaidi juu ya Klabu ya Simba kutokana na wivu wako kwa mafanikio iliyonayo na iliyoyapata.

Wewe ni Waziri wa hovyo mno katika hiyo Wizara ya Michezo na sijui hata kwanini 'Mkweo' ambaye ulimuudhi na kumkera sana kwa madudu uliyoyafanya katika wizara ya awali aliyokuweka na akaamua kukutupa huku kwetu GENTAMYCINE (michezoni), ambako hujui lolote lile na hukuwezi kabisa huku ukiwa unabahatisha bahatisha tu.
 
Back
Top Bottom