Viongozi wa Kamati ya Olimpiki waliwaahidi Wananchi kwamba nchi yetu itaushangaza ulimwengu katika michezo hii. Kwamba walifanya maandalizi na mazoezi ya kufa mtu, kuhakikisha wanarudi na medali nyingi. Kilichojitokeza ni kwamba wamewashangaza Wananchi, si Walimwengu, kwa mwenendo mbovu walio nao na si ajabu wakatoka mikono mitupu toka hiyo safari yao ya Utalii nchini Ufaransa. Sana tunashangazwa na Kisiwa cha St. Lucia chenye eneo la kilomita za mraba 617 na idadi ya watu 200,000 hivi kupata medali ya dhahabu ambayo ni ya kwanza kupitia mkimbiaji wao wa kike, Julien. Need I say more?