Waziri wa Nishati January Makamba afanya historia, Awasilisha Hotuba ya Bajeti yenye QR Code mara ya kwanza kwenye Historia ya Bunge la Tanzania!

Umeme wa kuchajia simu na vishikwambi vya kufungulia hotuba kwa QR code unapatikana kwa uhakika kila mahali?
Sifa zingine inabidi tumshangae mtoa sifa kama yupo sawa sawa kichwani au tumboni.
Maana mayala (njaa) ikizidi watu hupoteza uwezo wa kufikiri, wakipewa mlo toka kwa mikono michafu wanasifia hadi vitu vidogo sana.
 
Nimescroll down nione hata Q,R code ni some hiyo bajeti olaaa, ila tunasafiri ndefu sana kufikia nchi ya ahadi nimegundua tunawategemea watufikishe hao wenyewe hawataki kufika.
 
Makamba nachompendea anaejiamini na Yuko mbioni kutafuta Urais
 
Hata kama wanasema alikua mpigaji lakini alijua namna ya kula na kipofu kuna kitu alifanya hasa kwenye Rea, lakini huyu yeye anaingia tuu umeme umekua tatizo hadi kesho kutwa Kila siku matengenezo yasiyo malizika
Huyu kawekwa na mafisadi analinda maslahi ya mafisadi badala ya wananchi
 
Training tunazohudhuria huwa tunascan QR code,
Sioni Cha ajabu,
Cha kunifanya nianze kutoa sifa,
Kweli tupo nyuma mno🙆‍♀️
Hili nalo la kumsifia mtu kuwa yupo makini .
Hii ndio maana ya third world countries
 

Akili ni Muhimu sana, kwamba hiyo QR code kaigundua yeye? Katumia tu hela, full stop, Hakuna jipya. Sijui cha kusifia ni ni hapo!
 
Sawa endelea kupalilia mazao ipo siku utakumbukwa

Maana hiyo QR Code ni kitu cha kawaida Sana
 
Paskali- mengine sawa lakini hilo la mwisho kweny aya za mwisho HAPANA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…