Wanabodi,
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!.
Kabla hujasoma hoja za bandiko hili, naomba uanzie hapa kwa kuangalia hili ni bandiko la lini
January Makamba Top The List of Most Interactive Politician in Tanzania!
Sasa leo katika Bunge la Bajeti, Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba afanya historia ya matumizi ya ICT katika uwasilishaji wa bajeti, awasilisha hotuba ya bajeti yake ikiwa na QR Code, hii ikiwa ni mara ya kwanza kwenye Historia ya Bunge la Tanzania kwa hotuba ya bajeti yenye QR code.
Kwa faida ya wasiojua kuhusu QR Code, zamani hotuba za bajeti za Wizara zote na hoja zote zilikuwa zinaprintiwa hard copy, na kuwekwa pigeon holes za wabunge, this uses millions!.
Baada ya kuanza e-government, wabunge wote wamepewa vishkumbi, iPads, hotuba za bajeti zinakuwa kwenye soft copy, wabunge wanatakiwa kutembelea tovuti ya Wizara na kuipakuwa kwa kuidownload na kuisoma.
Kitendo cha kuwasilisha hotuba yenye QR code, sasa hakuna haja ya kumtumia mtu wala ku download, ni una scan tuu QR code, hotuba yote inafunguka kwenye kishkwambi chako au simu yako, hivyo saves time na hustles.
La mwisho ni January Makamba presentations ya bajeti yake, he was speaking like a president in waiting!.
I was very right niliposema hivi kumhusu
January Makamba, very intelligent, humble, down-to-earth! Can make the best President
Paskali