Ndugu Waziri wa Nishati, mheshimiwa Januari Makamba, ninakuandikia kwa masikitiko makubwa juu ya KERO YA UMEME wilayani Nkasi. Umeme unakatika mara kwa mara isivyo kawaida. Ni kero. Biashara za watu zinazotumia Nishati hii muhimu zimedorora na nyingine zimefungwa kabisa. Vifaa vingi vya umeme vinaungua majumbani mwa watu kila siku. Wananchi tunajiuliza, Tatizo lipo wapi? Tatizo lisiloisha! Umeme unawashwa dakika kumi unazimwa. Hivyo hivyo!
Je, ni Tatizo linalosababishwa na uchakavu wa vifaa? Upungufu mkubwa wa mafuta? Au ujuzi mdogo wa wahandisi na mafundi sanifu wa umeme?
Tunashauri: TANESCO walitafutie ufumbuzi wa kudumu Tatizo hili. Iwapo wamebaini Tatizo linalosababisha umeme kukatika-katika hovyo, Si wakae na kutengeneza kabisa hata kama itachukuwa miezi sita, na kadhalika, ili watakapowasha mitambo, Iwe moja kwa moja. Hii "danganya toto" haifai hata kidogo. Serikali inajivunjia heshima.
Mheshimiwa Makamba tunakuomba fuatilia shida hii Nkasi, Isije ikawa baadhi ya Watumishi wachache wa TANESCO wasio waaminifu wanahujumu juhudi za Serikali za kuhakikisha Nchi inatoka gizani. Wanakuharibia mheshimiwa. Ni mengi yasiyopendeza yameanza kusemwa juu ya kadhia hii; Si unajua hii ndiyo Wilaya pekee Nchini ina Jimbo linaongozwa kisiasa na Chama cha Upinzani? Wananchi wameanza na Kumkumbuka mbunge mstaafu Ally Mohamed Keissy; Inawezekana angekuwepo Bungeni haya yasingetokea.Tafadhali tusaidie Waziri. Wananchi Tunateseka.