DOKEZO Waziri wa TAMISEMI ingilia kati 'upigaji' wa fedha za kujikimu unaoendelea kwa Ajira Mpya

DOKEZO Waziri wa TAMISEMI ingilia kati 'upigaji' wa fedha za kujikimu unaoendelea kwa Ajira Mpya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

landibongo

Member
Joined
Mar 24, 2025
Posts
47
Reaction score
187
Waziri wa TAMISEMI ingilia kati rushwa na upigaji utoaji wa fedha za kujikimu kwa ajira mpya.

Ukifuatilia Halmashauri mara kwa mara wanakulipa cha kushangaza ni kwamba unapewa fedha pungufu wengi wamelipwa Tsh. 150,000.

Asilimia kubwa tangu January na February ajira mpya bado hawajalipwa kilichotokea ni wahusika kutengeneza mazingira ya mchakato kuwa mrefu ili watu wakate tamaa.

Mwishowe fedha wanazilipa kwa mafungu imefika pointi watu wanalipwa Shilingi 150,000 wakati minimum fedha ilikuwa Shilingi 1,000,000.

Muda mwingine ukijaribu kufuatilia fedha unaambulia vitisho na kejeli, Halmashauri nyingi wamelipa kwa wale waliosimama kidete kudai fedha za kujikimu japo fedha zimepunguzwa bila maelezo yoyote.

Wengine wanaombwa rushwa ili kupatiwa hizo fedha za kujikimu, kwa maelezo ya Waziri alishasema fedha tayari zimelipwa kwa hiyo atoke hadharani na kufafanua hii sintofahamu.

Jambo lingine ni kuwa Ajira mpya za Walimu Msingi na Sekondari Mwaka wa Fedha ulioisha hawajalipwa fedha za kujikimu tangu Februari 2025, Viongozi wakiulizwa hawatoi majibu ya kueleweka ni kusema tu mtalipwa.
 
Usikutee waziri mwenyewe hzo fedha anakata asilimia zake kadhaa Kwanzaa kabla yakuzitoa 😀😀😀, mfumo unaokabidhiwa nao unakata asilimia zake kadhaa ,mpk zijeziwafikiee wahusikaa n km hvyo laki na nusu 😀😀😀😀 ,
 
Halmashauri ya manispaa kigoma ujiji hawajalipa kabisa hii pesa ya kujikimu danadana zimekuwa nyingi sana sijui shida ni nini
 
Waziri wa tamisemi ingilia kati rushwa na upigaji utoaji wa fedha za kujikimu kwa ajira mpya
ajira mpya

Ukifuatlia halmashauri mara kwa mara wanakulipa .cha kushangaza ni kwamba unapewa fedha pungufu wengi wamelipwa 150,000

Asilimia kubwa tangu January ajira mpya bado hawajalipwa kilichotokea ni wahusika kutengeneza mazingira ya mchakato kua mrefu ili watu wakate tamaa

Mwishowe fedha wanazilipa kwa mafungu imefika point watu wanalipwa 150,000 wakati minimum fedha ilikua 1,000,000 .

Muda mwingine ukijaribu kufuatilia fedha unaambilia vitisho na kejeli halmashauri nyingi wamelipa kwa wale walio simama kidete kudai fedha za kujikimu japo fedha zimepunguzwa bila maelezo yeyote.

Wengine wanaombwa rushwa ili kupatiwa hizo fedha za kujikimu.

Kwa maelezo ya waziri alishasema fedha tayari zimelipwa kwa hiyo atoke hadharani na kufafanua hi sintofahamu
Dogo ni Bora ungefika ofisini na ukapewa ufafanuzi kuliko kupost kwenye mitandao inaonekana bado ujapewa orientation ya kutunza Siri za serikali
 
Dogo ni Bora ungefika ofisini na ukapewa ufafanuzi kuliko kupost kwenye mitandao inaonekana bado ujapewa orientation ya kutunza Siri za serikali
Siri gani acheni wizi toeni pesa za watu.

Mmezikalia pesa za watu kwa tamaa zenu halafu mnataka kutunziwa siri.
 
Hii ndio serikali ya chura a.k.a Dalali. Ni mwendo w kuwaibia watanzania. Ila zenji kwao mambo safi kabisa
Kazi ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom