Waziri wa Tamisemi toeni vibali vya kuajiri kwa waliojitolea kwenye ajira za mikataba ndani ya Halmashauri

Waziri wa Tamisemi toeni vibali vya kuajiri kwa waliojitolea kwenye ajira za mikataba ndani ya Halmashauri

KAUCHEZEA

Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
29
Reaction score
15
Mh. Waziri wetu,tunaomba muliangalie hili kwa jicho la kipekee,Vijana wamekubali kulitumikia Taifa Lao kwa uzalendo wa hali ya juu.Vijana kila mwaka wanapata ajira za mikataba,hii inaonyesha Kuna uhaba wa wafanyakazi ndani ya Halmashauri zetu.

Hivyo Kuna vijana wengi wanapewa ajira za mikataba Kama kazi za kukusanya mapata,udereva,Usafi wa mazingira pamoja na Ulinzi.

Njia nzuri ya kuboresha maisha yao Ni kuwapa ajira za kudumu kwani wanauzoefu mkubwa ndani ya Halmashauri zetu.Kazi za mkataba zinawanyima fursa nyingi za kuboresha maisha yao ya baadae hasa ya uzeeni kwani hakuna pensheni wala hawawezi kukopesheka.Vijana wengi wanaelimu na ujuzi ktk majukumu wanayopangiwa.

Hivyo ni jukumu sasa Waziri Ummy Mwalimu kushauriana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ili kuleta Suluhu ya tatizo ili ndani ya Halmashauri zetu.

Wapo vijana Wana Elimu ya degree,diploma na certificate lkn bado hawana ajira za kudumu na wamejitolea taklibani miaka 2 sasa na hawajui hatima yao ya kesho.

Na Imani kabisa Jambo hili litachukuliwa uzito wa kipekee ili vijana waweze kuhudumia Taifa lao kwa uzalendo zaidi.Mungu ibariki Tanzania,Mungu wabariki Viongozi wetu.Amina
 
Hahah yule jamaa alizalisha wazalendo feki sana aiseee.

Kijana una shida ya ajira ila umeona ujifiche nyuma ya neno uzalendo uchwara.
 
Back
Top Bottom