Waziri wa TAMISEMI tuondolee rushwa idara ya elimu

Waziri wa TAMISEMI tuondolee rushwa idara ya elimu

ambwilikiti

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2014
Posts
204
Reaction score
59
Tafadhali sana waziri wa Tamisemi George Mkuchika tuondolee rushwa halmashauri ya moshi!Watumishi wa idara ya Elimu Halmashauri ya Moshi tumechoka na vitendo vya rushwa vinavyozidi kushamiri siku hadi siku katika Halmashauri ya Moshi.

Tatizo linazidi kota mizizi, mf. ni Hiki kitendo cha hivi karibuni baadhi ya watumishi wa Halimashauri ya Moshi kuunda umoja wao lengo lao ni kujikusanyia fedha kwa njia za rushwa.

Mfano baadhi ya walimu waliambiwa watoe rushwa ya laki tatu hadi sita ili wapandishwe Madaraja/daraja kinyume na utaratibu yaani bila kutimiza msharti ya kazi km ilivyoagizwa kwenye waraka wa serikali juu ya upandishwaji wa madaraja kwa watumishi wa umma.

Pamoja na mambo mengine katika waraka ule inamzuia mwajiri(mkurugenzi kwa niaba ya serikali kuu) kuwapandisha watumishi kwa mkupuo na lazima mtumishi afanyiwe tathimini km form za opras zinavyoelekeza.

Cha kusikitisha baadhi ya watumishi wamepandishwa madaraja kinyume cha utaratibu(rejea majina ya walimu waliopandishwa madaraja hv punde) utagundua wenye sifa wengi wameachwa kwa kuwa hawakuwa tayari kutoa rushwa ya ngono ama laki sita ama vyote kawa pamoja.

Sasa Mh.waziri Mkuchika ile dhana ya utawala bora ipo wapi?

Watumishi kama hawa wanafanya mambo kiholela kama serikali imeenda likizo wakati tunajua mkono wa serikali ni mrefu?

Hii inaweza ikatufanya tuamini kuwa kuna wakubwa nao wanashiriki kula rushwa za wanyonge (walimu walioshindwa kutoa rushwa kwa kutambua ni kosa kisheria).

Rushwa adui wa haki

Kutokana na rushwa hiyo hiyo kunabaadhi ya watumishi watumishi walilipwa zaidi ya mara moja (baada ya kutoa rushwa) bahati nzuri hiyo ishu iligundulika hivyo wamewalazimisha waliolipwa kwa kile walichodai ni kimakosa waandike barua na wakiri na wajieleze watalipaje hela ya ziada waliyolipwa.

Hii ni aibu kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Moshi na waziri Mkuchika .INAKUWAJE UZEMBE KAMA HUU UNATOKEA HALAFU HALMASHAURI INASEMA "ETI NI BAHATI MBAYA" huku ikisababisha usumbufu mkubwa kwa walimu waliolipwa na hata kwa serikali kwa ujulma?

AU WANATAKA USEMI UTIMIE KUWA KUNA WATENDAJI NA MAWAZIRI MIZIGO?

Maana haiwezekani rushwa iote mizizi na hakuna hatua za dhati na za makusudi kuchukuliwa km vile kufanya uchunguzi wa kina hatimaye serikali ijiridhishe na itoe uamuzi mgumu na sio KUCHEKACHEKA na viongozi wazembe wenye kuichafua serikali na chama kwa ujumla.
 
I can't see some words normally !

The hell out there it's green colour !
 
Heh, unapenda kupoteza muda wako kweli. Of all the people wa kupambana na rushwa, Mkuchika? Tena mwana CCM!!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
poleni sie wa mtwara asante mungu unapanda kwa haki na hatuna rushwa karibuni mtwara mikindani
 
Takukuru hakuna hapo Moshi???!!!
Wekeni kila.kitu sehemu inayohusika then mnaanza na vyombo vya habari wakati mmefanya yote ya msingi!!!!

Hapa mtaambiwa kwa nini hamjapeleka Takukuru???!!!!
Kama wanawasumbua sana waambieni kuwa nanyi "mnaweza kuwasumbua" zamani hakukuwa na polisi wala mahakama ila jamii ilikuwa na adabu!!!!
 
TAMISEMI na Mkuchika wapi na wapi! Hawa Ghasia ndo mhusika wa TAMISEMI pamoja na Mwanri na Majaliwa wakiwa wasaidiz wake!
 
Heri nyie sisi tunapigwa sandakalawe tu! Ukistaajabu ya Moshi kuja Nachingwea ujionee shaghalabagala.
 
Waziri wa TAMISEMI ni Hawa Ghasia na Mkuchika ni Waziri wa nchi Utawala Bora. Ila naamini ujumbe wako umewafikia.
 
Back
Top Bottom