Waziri wa Ujenzi, Bashungwa Atoa Ufafanuzi Daraja la Kuunganisha Dar na Pwani: Litaanza Kutumika Kufikia Kesho Jioni

Waziri wa Ujenzi, Bashungwa Atoa Ufafanuzi Daraja la Kuunganisha Dar na Pwani: Litaanza Kutumika Kufikia Kesho Jioni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametoa ufafanuzi wa Changamoto iliyotokea katika daraja linalounganisha mkoa wa Pwani na Dar es salaam katika barabara ya Tegeta kuelekea Bagamoyo kwa kueleza kuwa timu ya wataalam imeshafika kufanya tathimini ya daraja hilo.

Bashungwa ametoa pole kwa Wananchi na watumiaji barabara hiyo kwa shida wanayoipa kutokana na kusitishwa kwa matumizi ya daraja hilo.

Amesema Serikali inafanya kila jitihada ya kuhakikisha kufikia kesho jioni ya tarehe 09 Disemba 2023 huduma ya barabara hiyo iwe imerejeshwa

Aidha, Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kupitia Mameneja wa mikoa kuhakikisha wanakagua madaraja na barabara zote mara kwa mara katika msimu huu wa mvua za El-nino.

 
Back
Top Bottom