Waziri wa Ulinzi aongoza waombolezaji kuaga mwili wa Meja Jenerali Gimonge (Mstaafu), Machi 13, 2024

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), Machi 13, 2024 ameongoza waombolezaji kuaga Mwili wa Marehemu Meja Jenerali Christopher Keraryo Gimonge (Mstaafu) katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Akitoa salamu za rambirambi Waziri Stergomena Tax aliwasilisha salamu za pole toka kwa Amri Jeshi Mkuu Daktari Samia Suluhu Hassan, kwa kusema kuwa Serikali pamoja na jeshi limepoteza Kamanda na Kiongozi muhimu kwani wakati wa uhai wake marehemu alitumikia jeshi katika nafasi mbalimbali kwa mafanikio makubwa ambapo ametoa wito wa kuiga yote mambo mema na uchapakazi aliounyesha Marehemu Meja Jenerali Gimonge (Mstaafu).

Viongozi wengine waliohudhuria tukio hilo ni pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Wakuu wa Majeshi Wastaafu, Majenerali, Maafisa Wakuu, Maafisa Wadogo, Askari pamoja na waombolezaji, ambapo mwili wa Meja Jenerali Gimonge umesafirishwa leo kwenda Mkoani Mara kwa maziko.




 
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) leo Machi 13, 2024 ameongoza Waombolezaji kuaga Mwili wa Marehemu Meja Jenerali Christopher Keraryo Gimonge (Mstaafu) katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo Jijini Dar Es salaam.




Akitoa salamu za rambirambi, Waziri Stergomena Tax aliwasilisha salaam za pole toka kwa Amri Jeshi Mkuu, Mhe Daktari Samia Suluhu Hassan,kwa kusema kuwa kuwa, Serikali pamoja na Jeshi limepoteza Kamanda na Kiongozi muhimu kwani wakati wa uhai wake, marehemu alilitumikia Jeshi katika nafasi mbalimbali kwa mafanikio makubwa ambapo ametoa wito wa kuiga yote mambo mema na uchapakazi aliounyesha marehemu Meja Jenerali Gimonge (Mstaafu)


Viongozi wengine waliohudhuria tukio hilo ni pamoja na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Luteni Jenerali Salum Haji Othman, Wakuu wa Majeshi Wastaafu, Majenerali, Maafisa Wakuu, Maafisa Wadogo, Askari pamoja na waombolezaji, ambapo mwili wa Meja Jenerali Gimonge umesafirishwa leo kwenda Mkoani Mara kwa maziko.
 
Apumzike kwa amani kamanda wetu.

Afande Gimonge wakati angali Luteni alikuwa kamanda machachari sana akiwaambia watu kuwa yeye alikuwa anatembea na masignecha ya rais kwenye mabega yake.

Alipokwenda vitani aliongozana na waliokuwa wanafunzi wake ambao baadaye wote walipanda kuwa majenerali, kwa mfano mmojawapo akiwa hayati General Martin Mwankanye.
 
Apumzike kwa amani General .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…