Waziri wa ulinzi atoa pole vifo na majeruhi ya wanajeshi wa tanzania, drc

Waziri wa ulinzi atoa pole vifo na majeruhi ya wanajeshi wa tanzania, drc

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt Stergomena Tax (Mb), atoa salamu za pole Kufuatia Vifo na Majeruhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania-JWTZ Walioko DRC.
 
Attachments

  • MOD PRESS release.mp4
    57 MB
..nchi za zilizostaarabika Wanajeshi wakifariki vitani habari zao hupewa nafasi kubwa kuliko habari zote ktk vyombo vya habari.

..Na mapokezi ya miili yao hupewa heshima kubwa na viongozi na vyombo vyote vya serikali na dola.
 
USA, UK
 
WAZIRI WA ULINZI ATOA POLE VIFO NA MAJERUHI YA WANAJESHI WA TANZANIA, DRC

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ametoa salamu za pole kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, kufuatia vifo vya Wanajeshi watatu (3) na wengine watatu (3) kujeruhiwa , kutokana na shambulio la Bomu wakati wakishiriki Misheni ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) nchini DRC

Katika taarifa yake, Waziri Tax, amesema Tanzania imepoteza mashujaa hao wakiwa katika majukumu ya kutafuta amani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tunawaombea mashujaa wetu Mungu awalaze pema peponi, na kuwaponya haraka majeruhi. Mashujaa wetu watapumzishwa kwa heshima zote kwa kuzingatia taratibu za Kijeshi.

Pia amelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kulinda amani, katika mipaka yetu na nje ya mipaka yetu kulingana na makubaliano na Itifaki za Kikanda na Kimataifa ambapo Tanzania ni mwanachama.

Aidha, ametoa pole kwa ndugu, jamaa na familia kwa kuondokewa na wapendwa wao ambao wamepoteza maisha katika kutafuta amani nchini DRC.
 
Attachments

  • IMG-20240409-WA0070.jpg
    IMG-20240409-WA0070.jpg
    31 KB · Views: 4
  • IMG-20240409-WA0069.jpg
    IMG-20240409-WA0069.jpg
    29.9 KB · Views: 6
..tulipoteza askari Congo na wengine waliouawa na magaidi lakini Jiwe hakushiriki kuwaaga.

..siku ya tukio la kuwaaga askari Jiwe alikwenda kufungua hosteli za wanafunzi wa chuo kikuu.
Kuwaaga ndio nini?
 
Bring back home wapiganaji wetu,kule wanapigana vita kwa faida ya nani?warudi nyumbani watulindie mipaka yetu hasa huu wa kusini ,hivi hawa wakongo nikiwauliza mnapigania nini wanaweza kuwa na jibu kweli?,wameamua kuuana tuwaache wauane
 
..nchi za zilizostaarabika Wanajeshi wakifariki vitani habari zao hupewa nafasi kubwa kuliko habari zote ktk vyombo vya habari.

..Na mapokezi ya miili yao hupewa heshima kubwa na viongozi na vyombo vyote vya serikali na dola.
Tanzania tunawapa vipaumbelw wakina mwijaku babalevel steve nyerere

Ova
 
Back
Top Bottom