Waziri wa usalama, IGP wapigwa faini ya Kshs. 200,000 kwa kudharau mahakama

Waziri wa usalama, IGP wapigwa faini ya Kshs. 200,000 kwa kudharau mahakama

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Mahakama Kuu nchini Kenya, imewapiga faini ya shilingi za Kenya 200,000, waziri wa mambo ya ndani Fred Matinag'i (mbele kushoto) na Inspekta jenerali Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet (hayupo pichani) kwa kosa la kudharau mahakama. Jaji George Odunga aliwaamuru maafisa hao waandamizi wa serikali kufika mahakamani siku ya Jumatano, kwa ajili ya kuhukumiwa, baada ya kutiwa hatiani kwa kudharau mahakama walipokataa kumuachia mwanasiasa wa upinzani Miguna Miguna. Odunga ameagiza pesa hizo zikatwe kwenye mishahara yao.


29683700_1932918210086830_141120912941025873_n.jpg


Chanzo: DW
 
Safi sana. Sio mahakama ya nchi ya ahadi, yenyewe ni hewala tu...
Huoni waziri na IGP wamedharau wito wa mahakama.

Pia huoni mahakama umezuia Miguna Miguna asifukuzwe lakini serikali wamemfukuza tena kimabavu, je uhuru wa mahakama upo wapi hapo?

Huo usafi unatokea wapi?
 
Baada ya kugomea amri ya mahakama, kilichofauatia ni nini? Pigwa faini tena itakayokatwa kwa mishahara zao.
Miguna Miguna katimuliwa kimabavu uku mahakama walikataza lakini serikali wamemfukuza tena kimabavu na kwa taarifa yako wamem drugged akiwa na afisa wa kijasusi.
 
Ubaya zitalipwa kwa hela za walipa kodi sio hela kutoka mfukoni mwa hao viongozi.
 
There is only jungle law in Africa...Why do we even try to have constitutions and institutions? A lot of African leaders are above the law...Welcome to Africa...
 
Back
Top Bottom