Waziri wa Utumushi, Mchengerwa: Maafisa utumishi wasiopandisha madaraja kutumbuliwa

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
Hizi mbwembwe za awamu ya sita zipo kasi sana, anyway, yetu macho na masikio.

===

"Watumishi wote waliosimamishwa kazi na mashauri yao yamechukua muda mrefu waandike barua kwa Katibu Mkuu Utumishi na aniletee nakala kwa ajili ya kufuatilia"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa"

"Kama nikisikia kama kuna mtumishi hajapandishwa daraja, nitamuondoa Afisa Utumishi huyo mara moja. Kama nikisikia kama kuna mtumishi hajapandishwa daraja wakati anastaili, nitamuondoa Afisa Utumishi huyo aliyemkwamisha mara mara moja. Haiwezekani mtumishi anaajiriwa leo, umempita miaka minne mnapokea mshahara sawa, haiwezekani. Serikali haitaki mtumishi wa umma aonewe, stahiki zenu ni haki yenu hampaswi kuziomba"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa

"Nikipita katika sehemu zangu za kazi, nikikuta kero za watumishi, watumishi wanaandika barua hajibiwi miezi sita. Aliyekuwa katika mamlaka yangu nitatengua nafasi yake. Aliye nje nitaomba mamlaka ya uteuzi wamtengue. Watumishi wa umma mjipange, wizara hii sasa imepata kijana. Bahati mbaya sijui nzuri nilikuwa hakimu, ninapenda haki. Tuwasikilize wananchi wanaofika katika ofisi zetu.

Nikikuta wamesimama wanasubiri kusikilizwa na anayepaswa kusikiliza hayupo, nitamsikiliza Mimi"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa

"Watumishi wote waliosimamishwa kazi na mashauri yao yamechukua muda mrefu waandike barua kwa Katibu Mkuu Utumishi na aniletee nakala kwa ajili ya kufuatilia"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa.

IMG_20210503_153756.jpg
 
Mh Waziri Kuna Uhamisho wa kukomoa...wapo watu huunda Njama na kuitumia Ofisi yako Unashangaa mtu anahamishiwa Halmashauri ili kumkomoa.

Kule Halmashauri kuna haja ya kupaboreshea Vitendea kazi ili Wakuu wenye chuki wasizotumie Halmashauri kama sehemu yao ya kukomoa watumishi
 
Je hawa maafisa utumish wanao hack mfumo wetu na kuweka makato mara mbili ya cwt unatusaidiaje tukuandikie barua
 
Hiyo kauli ya kulingana salary huku mmepishana kwa miaka 4-8 ya kazini, naomba uandike walaka kwa waajiri wote, ni tatizo kubwa mno.
 
Maswali:
1. Kwanini suala la kupandishwa madaraja lisiwe automatically?
Data zote za watumishi ziko kwenu.
2.Je, ni watumishi elfu 80 na ushehe tu ndio wanaostahili madaraja mapya?
Kama jibu yes, maana yake tayari maandalizi yalishafanyika sasa kwanini mtafute kiki kwa ma H.R?
Hapa kuna kauongo kanaandaliwa.
Haya ndio yale mauzauza ya Magufuli. Akishindwa jambo anamtafuta wa kumtumbua ili apate kiki
 
Maafisa utumishi siku hizi wanafanya kazi na mabenki! wamejigeuza mawakala......kuingiza makato ya mikopo ya watumishi kwenye "lausoni" sijuhi kuna kamisheni huwa wanapata maana wapo fasta saaana! ila kwenye kuangalia mafile ya watumishi kama wamepanda madaraja huwa hawana muda.
Kingine, maafisa utumishi wa halmashauri za wilaya huwa wana nidhamu sana ya kupandisha madaraja ila wale wa manispaa na majiji hao ndio miungu watu...usipotoa rushwa(pesa, ngono, nk) hupandi ng'o!
 
Maafisa utumishi wameanza kutuambia eti tupeleke barua za kuthibitishwa kazini na ilihali zipo kwenye faili za mtumishi hapo halmashauri😆😆,
Kazi za kiserikali huwa hazieleweki,unaweza ukamuuliza mwanao unaitwa Nani?🤔🤔

Mi nilitakiwa nipande daraja Mara mbili sijui watapiga mseleleko au mi ndo sielewi!!!
 
Hizi mbwembwe za awamu ya sita zipo kasi sana, anyway, yetu macho na masikio.

===

"Watumishi wote waliosimamishwa kazi na mashauri yao yamechukua muda mrefu waandike barua kwa Katibu Mkuu Utumishi na aniletee nakala kwa ajili ya kufuatilia"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa"

"Kama nikisikia kama kuna mtumishi hajapandishwa daraja, nitamuondoa Afisa Utumishi huyo mara moja. Kama nikisikia kama kuna mtumishi hajapandishwa daraja wakati anastaili, nitamuondoa Afisa Utumishi huyo aliyemkwamisha mara mara moja. Haiwezekani mtumishi anaajiriwa leo, umempita miaka minne mnapokea mshahara sawa, haiwezekani. Serikali haitaki mtumishi wa umma aonewe, stahiki zenu ni haki yenu hampaswi kuziomba"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa

"Nikipita katika sehemu zangu za kazi, nikikuta kero za watumishi, watumishi wanaandika barua hajibiwi miezi sita. Aliyekuwa katika mamlaka yangu nitatengua nafasi yake. Aliye nje nitaomba mamlaka ya uteuzi wamtengue. Watumishi wa umma mjipange, wizara hii sasa imepata kijana. Bahati mbaya sijui nzuri nilikuwa hakimu, ninapenda haki. Tuwasikilize wananchi wanaofika katika ofisi zetu.

Nikikuta wamesimama wanasubiri kusikilizwa na anayepaswa kusikiliza hayupo, nitamsikiliza Mimi"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa

"Watumishi wote waliosimamishwa kazi na mashauri yao yamechukua muda mrefu waandike barua kwa Katibu Mkuu Utumishi na aniletee nakala kwa ajili ya kufuatilia"Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Aanze na ADERA hapo ofsn kwake! amtoe ampeleke awe afsa utumishi lindi huko akapigwe vizuri na watumishi wenye hasira maana ana kiburi sana mpuuz huyo dada
 
Unaweza kunikuta hata hako kadaraja kamoja wanakutoa knock out
Maafisa utumishi wameanza kutuambia eti tupeleke barua za kuthibitishwa kazini na ilihali zipo kwenye faili za mtumishi hapo halmashauri😆😆,
Kazi za kiserikali huwa hazieleweki,unaweza ukamuuliza mwanao unaitwa Nani?🤔🤔

Mi nilitakiwa nipande daraja Mara mbili sijui watapiga mseleleko au mi ndo sielewi!!!
 
Mh Waziri, toa kauli pia ya watumishi waliokwamishwa kupanda madaraja baada ya kwenda kujiendeleza kielimu. Yaani mtu anazuiwa kupanda daraja kisa alienda kusoma. Mbaya zaidi alijilipia na pia aliruhusiwa na mwajiri kwenda kujiendeleza. Hii nayo hebu itazame.
 
Maswali:
1. Kwanini suala la kupandishwa madaraja lisiwe automatically?
Data zote za watumishi ziko kwenu.
2.Je, ni watumishi elfu 80 na ushehe tu ndio wanaostahili madaraja mapya?
Kama jibu yes, maana yake tayari maandalizi yalishafanyika sasa kwanini mtafute kiki kwa ma H.R?
Hapa kuna kauongo kanaandaliwa.
Haya ndio yale mauzauza ya Magufuli. Akishindwa jambo anamtafuta wa kumtumbua ili apate kiki
Mazuzu nyinyi hamnaga jema ht serikali ichukue hatua gani nzuri
 
Jaman, hivi inawezekana kulipwa malimbikizo ya mishahara bila kuandika barua ya kudai?
 
Uwezekano upo japo ni ngumu. Watakulipaje walati hawana pa kurejea mapunjo yako? Kifupi usipo lipwa stahikizako ni rahisi kwa wewe kukumbuka kuwa ulipunjwa kuliko inavyoweza kuwa rahisi kwa aliyekupunja.
 
Back
Top Bottom