Waziri wa Zamani Wa Ulinzi Wa Burundi Meja Jenerali Cyrille Ndayirukiye Amefariki Leo Akitumikia Kifungo Cha Maisha Jela

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Meja Jenerali Cyrille Ndayirukiye alihukumiwa kifungo cha maisha jela Januari 2016 kwa kuhusika jaribio la kuipindua Serikali ya Mwendazake Piere Nkurunziza.

Jaribio hilo lililoshindwa lilifanyika Mei 16,2015 wakati Mwendazake Piere Nkrunziza akihudhuria Kikao cha Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Majenerali wengine waliohusika na jaribio hilo la mapinduzi na ambao walihukumiwa kifungo cha maisha ni Zenon Ndabaneze, Nimenya Hermenegilde na Juvenal Niyungeko almaarufu Kiroho.

Taarifa zinadai kuwa Meja Jenerali Godefroid Niyombare aliyeongoza jaribio hilo la Mapinduzi alitorokea nchini Rwanda

FB_IMG_16192949058668080.jpg
 
Burundi wanavumisha vitu Sana aisee huyo Jenerali yupo wapi?
 
... hivi huko Burundi hakuna vyeo vingine vya kijeshi zaidi ya jenerali? Kila askari ni jenerali!
 
Nchi ndogo halafu maskini wamebaki ujuaji ujuaji tu. Si wote wajishughulishe na kilimo, ufugaji na uvuvi. Ni ndio njia pekee itawainua kiuchumi na mawazo ya kufikiria uzalishaji badala ya vita na umwagaji damu.
 
Meja Jenerali Cyrille Ndayirukiye alihukumiwa kifungo cha maisha jela Januari 2016 kwa kuhusika jaribio la kuipindua Serikali ya Mwendazake Piere Nkurunziza.

Jaribio hilo lililoshindwa lilifanyika Mei 16,2015 wakati Mwendazake Piere Nkrunziza akihudhuria Kikao cha Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Majenerali wengine waliohusika na jaribio hilo la mapinduzi na ambao walihukumiwa kifungo cha maisha ni Zenon Ndabaneze, Nimenya Hermenegilde na Juvenal Niyungeko almaarufu Kiroho.

Taarifa zinadai kuwa Meja Jenerali Godefroid Niyombare aliyeongoza jaribio hilo la Mapinduzi alitorokea nchini Rwanda

View attachment 1762956
Hii ni picha yake?? Mbona hana cheo na red cola
 
Burundi Majenerali ni wengi kuliko Makoplo

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Vyeo vinatolewa kwa asante badala ya merits. Overstaffing ni kikwazo mojawapo kiliifanya Ukraine isijiunge NATO. Mna majamaa yameshika ramani uko ofisini na mengi ni incompetent yamepewa vyeo kama asante au kama 'utaratibu unavyosema'.
 
Back
Top Bottom