Waziri Zanzibar aeleza WhatsApp ilivyoendesha Wizara alipougua Covid19

Waziri Zanzibar aeleza WhatsApp ilivyoendesha Wizara alipougua Covid19

Rahma Salum

Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
30
Reaction score
59
Riziki Pembe, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ameeleza namna ambavyo Wizara ilivyokuwa ikiendelea na shughuli zake pindi alipokuwa hospitali kwa matibabu ya maambukizi ya Corona.

Waziri huyo amesema alikuwa akiwasiliana kupitia mtandao wa WhatsApp na viongozi wenzake, akiwemo Naibu Waziri, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi wote. Vilevile, amesema kuwa hakuna kazi yoyote iliyoharibika katika kipindi chote alichokuwa hospitali.

“Tumefanya kazi zetu zaidi kwa kupigiana simu na kupeana maelekezo ya kazi na kujibu maswali, kwa mfano watendaji wangu wengi walikuwa wanawasiliana na mimi kwa simu na kuwapa maelekezo na walikuwa wakitekeleza.” Ameongeza

Riziki ni mmoja wa viongozi walioambukizwa ugonjwa wa Corona alipokuwa katika safari ya kikazi nchi za Ulaya wakati ambapo COVID19 ilishika kasi katika mataifa mbalimbali duniani. Aidha ameeleza kuwa aliporejea nchini kutoka katika ziara ya kikazi hakuonesha ishara yoyote ya Corona. baadae alianza kupata dalili kidogokidogo kama kichwa kuuma na mwili kupata joto la juu.
 
Back
Top Bottom