Waziri Zungu: Mitumba inachafua mazingira

Waziri Zungu: Mitumba inachafua mazingira

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074
Nikushukuru sana Rais kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri, wakati nakuja Watu waliniuliza utavaa nguo zako za mitumba au utavaa kitu kipya, lakini leo nimetia suti mpya, maana hata hiyo mitumba ni sehemu ya mazingira na ni sehemu ambayo inachafua hadhi ya Nchi yetu.

Rais Magufuli umefanikiwa sana kupiga vita mifuko ya Plastic, lakini sasa mifuko hiyo inarudi kwa njia za pembeni, vifungashio (packages) sasa vinaboreshwa na Watu wanabebea vitu na kuharibu mazingira, watu wa NEMC tuulize kwanini vitu hivi viko mitaani, nitalifanyia kazi.

Kwa Watu wa Wizarani (Muungano na Mazingira) urafiki upo lakini kwenye kazi za Umma hatutofanya urafiki, tukikutana nje ya kazi za Umma tutaendelea na Urafiki wetu.

Amakweli mwenye shibe kamwe hamjui mwenye njaaa sasa tusubiri mapya ya kupiga marufuku mitumba.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa Huseein Mwinyi huyo jamaa sijui hayo malezi ameyapata wapi ya kuwa muungwana pamoja na kuwa na cheo kikubwa.

Sijawahi kumsikia kabisa akiongea maneno ya kujitweza kabisa.
Kaanza kushiba baada ya Bashe na Husein Mwinyi ndiye mtu angalau nilikuwa namwamini anaweza kuwa waziri mzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo 27/01/2020 baada ya kuapishwa Waziri Mpya wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Hassan Zungu alisema yafuatayo, "Nikushukuru Rais kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri. Wakati nakuja watu waliniuliza utavaa nguo zako za mitumba au utavaa kitu kipya, lakini leo nimetia suti mpya, maana hata hiyo mitumba ni sehemu ya mazingira na ni sehemu ambayo inachafua hadhi ya nchi yetu.

Mavazi ya mtumba husaidia Watanzania wenye maisha ya kati na duni kujisitiri, si hivyo tu baadhi yake hukaribia ubora wa yale mavazi mapya.Je Waziri alikuwa sahihi? Ama itakuwa sahihi kuzuia nguo hizi?Tuchukue hatua zipi?

Karibuni wana JF.
 
Back
Top Bottom