Waziri Zungu: Mitumba inachafua mazingira

Waziri Zungu: Mitumba inachafua mazingira

Hakika viongozi wetu hawana hata nafasi ya kuyasoma yaliyo wapata watangulizi wao
Haa[emoji28][emoji1][emoji2][emoji23][emoji16][emoji16][emoji3][emoji2][emoji2][emoji39][emoji39][emoji8]
Tujiandae Kuvaa Suti Nchi Nzima Kuanzia
Mjini Hadi Vijijini, Subira Inahitajika Unapopewa Cheo Ama Nafasi. Mengine Yanakera Yanachefua Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yule lugola alikua anasema magufuli zinyeme au zisinyeme huku akitingisha tako na bado katolewa huyu zungu anafahamu mitumba ni biashara kubwa na kuiondoa ni process ndefu hadi uwe na viwanda vya nguo vya kutosha nchini, na anafahamu kama mtumba ni biashara ya mataifa ya magharibi na anafahamu kua hiyo ni biashara ya wanyonge?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Leo 27/01/2020 baada ya kuapishwa Waziri Mpya wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Hassan Zungu alisema yafuatayo, "Nikushukuru Rais kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri. Wakati nakuja watu waliniuliza utavaa nguo zako za mitumba au utavaa kitu kipya, lakini leo nimetia suti mpya, maana hata hiyo mitumba ni sehemu ya mazingira na ni sehemu ambayo inachafua hadhi ya nchi yetu.

Mavazi ya mtumba husaidia Watanzania wenye maisha ya kati na duni kujisitiri, si hivyo tu baadhi yake hukaribia ubora wa yale mavazi mapya.Je Waziri alikuwa sahihi? Ama itakuwa sahihi kuzuia nguo hizi?Tuchukue hatua zipi?

Karibuni wana JF.
tuzuie kwanza kuongozwa na vyama chakavu
 
Suala la mitumba serikali inatakiwa kua makini sana nalo. Kimsingi kama jumuiya EAC member state walishakubaliana siku nyingi zilizopita kupiga marufuku mitumba. Rwanda walifanikiwa kwa 100% ingawa waliwekewa vikwazo vya kiuchumi na Marekani mpaka leo ingawa havina makali kihivyo. Tanzania ilijaribu kupandisha kodi mara kwa mara serikali nadhani ilidhani wafanyabiashara wataacha wenywe. Kontena ilikua inalipiwa ushuru wa 15M ikapanda nadha kwa sasa kontena moja inalipiwa ushuru wa 90M lakini watu wanaingiza mitumba kama kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hili waziri kachemka sana,sioni sababu ya kuzuia mitumba,nadhani waziri yeye anapokuwa na uwezo wa kuvaa suti basi watz wote wako hivyo,hapana kwa hili tumkemee huyu bwana,ukienda kwenye maguli/solo/ minada ya nguo utakuta asilimia 80 ya nguo zilizopo ni mitumba

Richa ya hayo viwanda vyetu bado havina uwezo wa kuzalisha nguo kwa mahitaji ya wa Tanzanialakini pia nguo za spesho zinagharama kubwa kuliko za mitumba ambapo kwa shilingi miambili mtu ana vaaa nguo,sasa hapa kwa watanzania wa kipato cha chini wajiandae kutembea matako wazi,waziri asidhani kuvaa suti kwa kodi za watanzania basi aamini kuwa watanzania wote wanao uwezo wa kuvaa suti au kununua nguo za spesheli

Yaani kwa mawaziri wenye mawazo mafinyu kama huyu watampa tabu sana rais ,maana full kukurupuka



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mitumba sio nguo tu,kuna Magari,vyombo/ vifaa vya umeme,vifaa vya kutumia majumbani/jikoni,viatu,mikanda,mikoba,midori,baskeli n.k

Ni vizuri uwepo utaratibu wa grades za mitumba hasa nguo ili zisiletwe zilizochakaa (grade za mwisho) na kama zitakuwepo kwenye marobota utengenezwe utaratibu wa kuzichoma.

Mbali na kutoa ajira kwa vijana (utajiri) nchini,mitumba imewafirisi vijana wengi na kusababisha wengine kuuza grades za mwisho zisizofaa kwa wananchi ili warejeshe mitaji yao.

Ni fedheha kuvaa mitumba,ingawa inasaidia kubana matumizi ya gharama za maisha kwani sio wote wenye uwezo wa kununua vitu vipya vyenye ubora wa nguo za mitumba kiupya kutokana na gharama kubwa.
mfano nguo za watoto hasa kuanzia umri wa1day-15yrs.

Kupigwa marufuku nguo za mitumba kutapingana na agizo la Mh.Rais la kuhimiza Watanzania kuzaana na kuongezeka ili uchumi tupate soko la bidhaa,otherwise mkakati madhubuti wa kufufua viwanda vya nguo mpya zinazoendana na ubora wa nguo za mitumba kiupya wake kabla ya kuwa mitumba uzingatiwe.

Sambamba na hivyo mkakati mahsusi wa uanzishwaji wa vazi la Taifa nao uendane na hatua za ama kuondoa/kupunguza nguo za mitumba ili Watanzania watu wazima waone fahari ya kuvaa vazi la nchi yao kuliko kukimbilia uvaaji ambao unaruhusu uagizaji wa nguo za mitumba.(provisional of public dress codes)
 
Kama kayasema hayo!! Basi kishashiba kabla hajala na hii ni hatari kubwa
 
Back
Top Bottom