Wazo bunifu: Ma IT wa JF

Nishafikiria sana idea hii

Kuna apps naona pia zinafanya, ila wanashindwa kumskip dalali, yani ukishapata nyumba kwenye app then kuinitiate communication inakupeleka kwa dalali
Ni ngumu kumskip madalali maana ndio wananyumba. Nimeona niwape sapot ili kupata wateja wengi kwa mkupuo . Wenye nyumba wengi wanaendeshewa nyumba zao na madalali.
 
Nice business idea bro. Shida ni pesa bro. Inawezekana sana babuu.
 
Ishu ni simple sana bro wala usichome calories nying kuhusu escrow. Kama umeshawai kutumia tigo web payment au gateway yoyote ya mitandao ya simu kuna kitu kinaitwa collection account na disbursment account.

Hii disbursment account ni mfumo ambao unaweza kumtumia mtu pesa au ukamrefund pesa au unaweza tuma malipo kwa watu wote wanaostail kulipa kila mwezi.

Escrow ni mfumo ambao wewe unaweza ukaungeneza kwenye system yako ili buyer na seller wasiwe na nguvu ya kutapeliana.

Kama pesa inaingia kwenye account ya kampuni maana yake buyer na seller hawana uwezo wa kuitoa ila wewe. Kitendo cha wewe kuhiruhusu iende kwa buyer au seller ndio escrow yenyewe hiyo bro.

Nilishawai fanya kazi na tigo najua hizo mambo nilizotaja hapo juu. Pia najua nini maana ya escrow , escrow ni ishu ambayo nimeojulia kwenye crypto p2p.
 
Nitajaribu kuongea nao. Kama nilivyosema hapo nyuma, ikishindikana kwa sasa, nitafanya employer wa-post kazi bila deposits yoyote. Labda baadae nita upgrade once hiyo huduma ikitokea.

Thanks.
Utakwenda kufeli . Kuna jamaa angu alitengeneza app ya usafirishaji bila nalipo kafeli swafi bila mbambamba.
 
Ni ngumu kumskip madalali maana ndio wananyumba. Nimeona niwape sapot ili kupata wateja wengi kwa mkupuo . Wenye nyumba wengi wanaendeshewa nyumba zao na madalali.
Mimi kwenye ku scratch kuna mwanga nimeuona kwamba dalali anaweza kuwa skipped, nadhani skipping dalali ndo disruption yenyewe difference ilipo mkuu.. sio asilimia mia kwa sasa ila nafikiri there is a way
 

Nashukuru kwa ku-share uzoefu wako. Changamoto ambayo najaribu kuepuka hapa au iwe very minimal, ni interaction ya mimi na app/system on a daily basis.

Kikubwa ninachotaka app/system iweze kufanya ni "Mwajiri aki-approve kazi baada ya kuridhika," malipo yafanyike automatically.

Kwa hiyo swali langu ni je, hilo linawezekana ukiwa na hiyo disbursment account?
 
YES.
 
Mimi kwenye ku scratch kuna mwanga nimeuona kwamba dalali anaweza kuwa skipped, nadhani skipping dalali ndo disruption yenyewe difference ilipo mkuu.. sio asilimia mia kwa sasa ila nafikiri there is a way
Labda ufanye property management, hapo ndipo madalali unaweza kuwakalisha vingunguti.
 
Kama unafanya kazi kwenye kiwanda chochote cha construction material such as cement, tiles, gypsum n.k. Naomba namba yako DM.

Kuna section nataka niweke kwenye mfumo watu tuwe tunanunua bidhaa za ujenzi kwa discount , kwa jina maarufu wanaita GROUP BUYING/ TEAM BUYING. Hapa natafuta vendors wakufanya nao kazi.

Lengo ni kupunguza gharama ya ujenzi kwa tunaoanza kujenga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…