Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
WAZO: FOMU YA MAKAZI NA HATI YA MKAZI KIDIGITALI. FAIDA ZA KIUSALAMA NA KIMAPATO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Niliwahi kuandika hapa mwaka Juzi, nikasema wanaolipa Kodi nchi hii ya Tanzania hawazidi Milioni Tatu. Nikiwa nazungumzia wale wanaotoa Direct Tax.
Mimi nikiwa mmojawapo.
Watu wakaja hapa, oooh! Wewe sio chombo cha Takwimu sijui. Ooh! Acha Mawazo mgando. Ooh! Ukamatwe utoe Maelezo. Mwaka Jana wahusika wenyewe wakatoa Takwimu Zao ambazo hazikuwa mbali na kile nilichosema, yaani ni mulemule.
Huwezi kukusanya Kodi kwa Watu wasiorasmi. Sasa utakusanyaje?
Watu pekee ambao unaweza kukusanya Kodi ni watu Rasmi wanaofanya shughuli Rasmi.
Nikasema, serikali lazima iandae Mpango mkakati wa Kurasimisha watu na MAKAZI Yao. Ambapo mchakato huo umefanyika kwa sehemu, watu kupewa Kitambulisho cha uraia ni sehemu ya Urasimishaji WA watu.
Lakini pia Mwaka Jana kama sio mwaka juzi Serikali iliendesha zoezi la Kurasimisha MAKAZI ya watu. Ni Hatua nzuri.
Sasa Leo tunazungumzia kuunganisha Urasimishaji wa Watu + Urasimishaji WA MAKAZI. Ambapo ili kuwe na ufanisi lazima Mpango na mkakati ufanyike kujua;
Mipango Mahususi
1. MAKAZI Fulani kuna watu wangapi, jinsia wapo wangapi, na ni kina Nani na wanafanya shughuli gani?
2. Kujua ongezo la watu Kwa kuzaliwa na kuhamia.
3. Kuratibu shughuli za mipango miji
4. Ulinzi na usalama
MPANGO MKUU;
KUBORESHA MAISHA YA WATU NA UKUSANYAJI WA KODI
MIKAKATI;
1. Kutoa Namba za Nida na kitambulisho cha taifa kwa kila Mtanzania
2. Kuunganisha Namba za Nida na Tin Number
3. Kila Mtanzania anayemaliza shule iwe mwenye umri wa Miaka 18 apewe Tin Number Akiwa shuleni wakati anamaliza Masomo yake. Hii ni Kwa sababu kulingana na Mtaala wa sasa hakuna mtoto atakayemaliza shule Akiwa chini ya miaka 18.
4. Serikali iunde Data base na kutengeneza application itakayotumika na serikali za mitaa kusajili Watu na MAKAZI Yao.
Application hiyo iwe na sehemu Mbili,
1. Sehemu ya Mwenye Nyumba
2. Sehemu ya Mpangaji
4.1. kila mtu anapoenda Kuishi sehemu yoyote Tanzania lazima asajiliwe na ofisi za serikali za mitaa na taarifa zake ziwekwe kwenye application kwa matumiz ya serikali tuu.
Taarifa za muhimu za mtu zichukuliwe ambapo nyingine zitatokana na namba ya NIDA.
4.2. Wageni wanaokuja kwa wakazi wa eneo husika. Wao hawatakuwa na haja ya kusajiliwa. Ila wenyeji wao ndio watakuwa wadhamini wao kwa Jambo lolote litakalo tokea.
Mfano. Taikon Master nimeenda Mikoani Kagera, Ngara kwa ngara23 nimeenda labda kusalimia, au kufanya shughuli fulani ya muda mfupi na nikafikia kwa mwenyeji wangu. Basi sitakuwa na haja ya kusajiliwa na taarifa zangu hazitakuwa na haja ya kuchukuliwa kwani mwenyeji wangu ngara23 ndiye atakuwa mdhamini wangu na atakuwa na taarifa zangu. Hii itamaanisha kuwa mwenyeji hatoweza kumpokea mtu mgeni asiyemjua.
4.2. Nyumba za Wageni zitakuwa na wajibu wa kuchukua taarifa za msingi ikiwemo vitambulisho vya taifa au leseni au hati ya kusafiria.
5. Kila MKAZI wa eneo husika mwenye Miaka kuanzia Miaka 20 ambaye sio mwanafunzi atatakiwa kulipia Tin number yake kila Mwaka Tsh 10,000 kwaajili ya maendeleo ya eneo analoishi ikiwa ni pamoja na barabara za ndani za mtaani kama zimeharibiwa na mvua, utunzaji wa mazingira ambapo kila mtaa lazima uajiri vijana wa kupanda miti na bustani na kuitunza. Ili mazingira yawe Safi.
5.1. Kodi ya serikali kuu itatokana na faida inayotokana na mapato ya shughuli anayofanya Mtu
6. Wanaoajiriwa Serikali za mitaa au kuchaguliwa wawe na vigezo vitakavyowafanya wawe Multipurpose. Isiwe kila mtu anaweza kugombea.
6.1. Mtu yeyote aliyesomea Community Development, Ukusanyaji wa Kodi ngazi ya cheti au stashahada, na kozi zozote za uongozi, sheria na usimamizi wa watu na fedha hao ndio waajiriwe kama maafisa utendaji na kuwania nafasi za uenyekiti Kata.
6.2. Majukumu ya Wenyeviti na watendaji(wenye vigezo nilivyovitaja kwa kifupi hapo juu) waongezewe jukumu la kufuatilia Wafanyabiashara wanaofanya kazi katika maeneo Yao kwamba wanalipa kodi inavyotakiwa. Hii itaanda sambamba na kuongezewa posho na maslahi Yao kulingana na Sheria na kanuni na madaraja Yao ya kielimu
6.3. Lisiwe jukumu la mlipa Kodi kwenda kutoa Kodi bali liwe jukumu la serikali kwenda kukusanya Kodi kwani imeajiriwa watu Kwa Kazi hiyo ya kukusanya Kodi.
6.4. bila kuathiri kifungu 6.3, serikali itakuwa na jukumu la kukusanya Kodi kwa kutumia mifumo ya kidijitali. Hii inamaanisha, kama serikali imeweka mfumo wa kulipa Kodi kwa Njia ya kidijitali haitakuwa na haja ya kuja kwa mfanyabiashara kuja kukusanya Kodi. Isipokuwa serikali itakuwa na jukumu la kwenda kwa wafanyabiashara kukusanya Kodi(maeneo yasiyo na mfumo wa kidijitali), kukagua biashara na kukadiria Kodi, kutoa ushauri n.k.
6.5. Mtendaji au Mwenyekiti ambaye ataruhusu mtaa wake ianzishwe biashara kiholela bila kufuata Sheria achukuliwe hatua.
Hii itamanisha, litakuwa jukumu la mtendaji na Mwenyekiti wa mtaa kujua shughuli za kijamii, kiuchumi zinazoendelea katika mtaa wake na kuhakikisha zinalipa Kodi.
7. Serikali Kuu itakuwa inatuma wakaguzi mara Moja moja kwa kushtukiza kukagua walipa Kodi katika mitaa.
Na mtaa wowote ambao atatokea mfanyabiashara asiyelipa kodi atakayechukuliwa Hatua atakuwa Mwenyekiti au mtendaji WA eneo husika.
7. 1 Hii itamaanisha, watu wote, wafanyabiashara ambao watakiuka kulipa Kodi lazima Watendaji au Wenyeviti watakuwa wameshaandika barua na vielelezo na taratibu zingine za kisheria kufuatwa ili Lisiwe kosa la Watendaji na wenyeviti.
8. Kazi zenye pato chini ya Laki tatu kwa mwezi. Serikali ikadirie Kodi ya elfu 30 kwa Mwaka.
Kazi zisizo Rasmi kama Bodaboda, mama Ntilie, Ususi, ufundi nguo, Ukinyozi, Usafisha kucha. Zote zirasimishwe.
Ni jukumu la serikali hasa ya mtaa kujua wakazi wake wanafanya shughuli gani.
8.1. vijiwe vyote vya Bodaboda kila mtaa visajiliwe na bodaboda wote wapewe Tin number number kisha conttol number ya kulipia. Isiwe lazima kulipia Tsh 30k yote kwa pamoja. Haya kidogokidogo ilimradi mwisho wa mwaka iwe imelipwa 30k. Halikadhalika na Wasusi na mama Ntilie.
Hivyo Mtu wa Mapato akifika kwa bodaboda au mtu atatoa kitambulisho chake na kujitambulisha, atamwomba bodaboda number yake ya NIDA na Tin number ili aingie kwenye mfumo kuangalia Kama Mhusika kalipa Kodi au laa
9. Kwa Kazi za uzalishaji wa Kilimo, Ni jukumu la serikali la kijiji akiwepo Mwenyekiti na mtendaji kuchukua sehemu ya kumi ya uzalishaji wa Mtu iende serikali kuu.
Mfano kama Mtu kavuna Debe moja itampasa atoe kilo mbili ziende serikalini.
Kama ni mfugaji, sehemu ya kumi ya mifugo na mazao ya Kilimo yanayozaliwa yaende serikalini.
Ni jukumu la serikali kusimamia Hilo na kuhakikisha linetekelezeka.
Ingawaje ni Kazi ngumu lakini ikiwekwa mipango na mikakati mizuri ya utekelezaji itachukua Muda mfupi kufanikisha hili.
Elimu itolewe.
Zaidi; ni jukumu la serikali kuhakikisha kila mtu ndani ya nchi anatumia ujuzi, kipaji na karama zake kuzalisha Mali na kipato ili kupunguza utegemezi.
Wanawake nao wote waliofikisha umri WA kufanya Kazi wafanye Kazi ili kupunguza utegemezi. Wanawake ni zaidi ya nusu ya watu wetu hapa nchini. Kuendekeza mitazamo ya kijinga na kimaskini na kuwafanya wao wahudumiwe tuu inaongeza utegemezi kwa asilimia hamsini bado, watoto, bado wazee, bado wagonjwa, bado waliojela, bado wavivu. Hatuna haja ya kupoteza nguvu Kazi ya nchi kwa kushikilia Mila potofu.
Haki Sawa katika kugawana mali zibainishwe na ziwe na HAKI.
Kile alichozalisha Mtu ndicho apewe siku ndoa ikivurugana na watu wakitalakiana.
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi.
Kwa sasa Dar es salaam