PostGE2025 Wazo Fyatu: Wamezoea Siasa za Kulipana, Hawaamini Kukataliwa!

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hawa wapumbavu karibu watuingize kwenye vita ya udini

Tutashukuru Mungu amewapa Gen z akili wakakwepa huo mtego

Kwa sasa wanawavunja moyo kwamba wamelipwa
 
 
Kazi aliyopewa Pm ni ngumu sana bila kukiri na kuwajibika kwa mauaji ya halaiki walioruhusu kwa maslah yao wenyewe!
 
Wanachojaribu kusema ni kuwa kuna watu wachache wamelipwa ili wachochee wengine. Ndiyo ile dhana waliyoipenyeza mwanzo ya "vijana kufuata mkumbo".

Upo sahihi kwa upande mmoja kwamba kwa kuwa wao wamekuwa wanatumia pesa kama silaha kwa muda mrefu, wanadhani pesa ndiyo inamsukuma kila mtu. Nadhani wanacheza tu siasa chafu za kuhadaa watu.

Ukiwafinya vizuri watakiri wanachosema hakina ukweli wowote ila wanaamini asilimia fulani ya watu wanaweza kuamini wanachosema kwa hiyo labda watavunjika moyo kwa kudhani kuna watu wanalipwa kuwachochea.

Wakija kugundua tulipofika hauwezi kukatisha watu tamaa kwa kuwahadaa kwamba wengine wamelipwa, watakuwa wamechelewa sana.
 
Mzee Mwanakijiji Kuna ''state of denial'' ambayo ni tatizo kuliko tatizo lenyewe. Kuna kutojielewa ''discombobulated'' kwasababu ya kuishi kwa mazoea bila kufikiri uwepo wa nyakati zinazopita. Mbinu alizotumia Mwinyi etc hazifanyi kazi tena.
Kwa kutojielewa ''Watu'' hawajishughulishi kutafuta chanzo, wanatafuta mahali pa kushika tu!

Tuliambiwa kuna watu wenye mabomu wameingia kupitia mpaka wa kaskazini! hawajashtakiwa hadi leo
Tukaambiwa vijana kutoka nchi jirani. Walioachiwa majuzi ni Watanzania, waliopo magereza ni Watanzania
Tukaambiwa Wanaharakati walioko nje wanachochea ! tukauliza kwa ushawishi upi kuliko serikali yenye vyombo
Tukaambiwa kuna vijana wamelipwa ! hakuna ushahidi na hakuna aliytetajwa achilia mbali kushtakiwa
Tukaambiwa kuna ''Waziri'' anapita kusikiliza maoni ya vijana! Vijana hao ni Watanzania si wa nchi jirani
Tukaambiwa kuna tume inayotakiwa kuleta majibu Vijana wanakosa haki gani! Ni Vijana wa Tanzania si nchi za nje

Tumesomewa orodha ya Bajaji na boda boda zilizoharibika, hatukuambiwa waliofariki au vituo vya kura vilivyoharibiwa. Wale wale walioshindwa kutueleza wanataka tuamini kuna mtu kapewa bilioni 5.

Ni mwendo wa ramli kila uchao! Kila ramli inamajibu tofauti kwasababu waganga ni wengi kila mmoja anataka uluwa wake. Hakuna mganga au kigagula anayetueleza chanzo cha matatizo. By the way ni kweli kwamba kwani hatujui chanzo? Ukipitia nyuzi za JF wengi walionya hatari kabla ya Oct 29. Watu wetu wakatafuta solution, fungia JF miezi 3. Niliwahi kumsikia mtu mmoja wa dini akisema ''watu wetu wana angamia kwa kukosa maarifa''

JokaKuu
 
This is beyond denial...I believe wameongezea cover up....wakitamka ukweli kwa vinywa vyao watakuwa wamejichongea wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…