Wazo Gomvi: Kabla ya Kujitoa CHADEMA Ingeeleza Hili Kwanza...

Wazo Gomvi: Kabla ya Kujitoa CHADEMA Ingeeleza Hili Kwanza...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Binafsi sina tatizo la kinadharia kwa CHADEMA kujitoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Na hata sitakuwa na shida ya msingi hata wakijitoa Uchaguzi Mkuu. Tangu zamani nilikuwa naamini kuwa kama unaona hutendewi haki ni lazima uoneshe kuwa kweli unaamini hakuna haki. Baadhi ya matatizo ambayo yametokea mara kwa mara - na sijui kama watu wamesahau au la - ni kuwa mara nyingi CHADEMA wanajikuta wanabanwa kwenye "masuala ya kiufundi" (technicalities).

- Kuchelewa kurudisha fomu hadi siku ya mwisho, saa ya mwisho
- Kuchelewa kula kiapo, au kula kiapo kisicho sahihi (nakumbuka sana kilichotokea Mbeya Vijijini mwaka uleeee)
- Kutokujua wanarudisha fomu kwa nani (Korogwe)
- n.k

Sasa, ni lazima tujue kuwa CCM na Serikali yake hawajawahi kuwa na mpango wa kutengeneza mazingira ya Upinzani kufanikiwa. Hili nimeliandika mara nyingi huko nyuma haifai kulirudia. Sijui kwanini wapo wanaofikiria kuwa Papa atajikata, atoe mafuta yake, akuwekee moto na sufuria, halafu ajitumbukize wewe kazi yako iwe kumkaanga tu! Sikumbuki mahali popote hili limewahi kutokea. Kutegemea CCM kuwasaidia wapinzani kuja kuwaondoa madarakani ni ndoto za Alinacha.

Baada ya kusema hilo, kufuatia uamuzi huu wa Chadema kujitoa kwenye kushiriki binafsi nilitarajia mambo kadhaa yangeelezwa kwanza, maana tusije tukawalaumu wasimamizi wa uchaguzi n.k kwa makosa ambayo yangeweza kuepukika. Kwa anayejua naomba atusaidie:

1. Ni nani alikuwa Mratibu wa CHADEMA wa wagombea wa nafasi mbalimbali serikali za mitaa kitaifa?

2. Huyo mtu/watu alitoa maelekezo gani kwa wanachama wa CDM kuhusiana na ujazaji wa fomu, kurudisha fomu n.k?

3. Je, CDM kitaifa ilitoa mwongozo gani kuhusiana na wagombea wake; kwamba wanahitaji nini na wajazaje fomu? Hii inaitwa "covering all your bases)

4. Hata mahali ambapo mikutano ya ndani isingewezekana CDM kitaifa ilifanya juhudi gani hata kupitia mitandao ya kijamii (Facebook, Youtube, au hata hapa JF) kuwajulisha wagombea wake jinsi ya kujaza fomu n.k Yaani, Freeman Mbowe au Katibu Mkuu Mashinji wameshindwa kuanzisha hata thread moja yenye maelekezo na nakala za fomu za mfano za nini kinatakiwa zikawekwa hapa?

5. CDM iliwaandaa watu wake vipi kubanana na wale wasimamizi ambao walikuwa wanaonekana kweli kuwakwepa. Hivi kweli CDM na vijana wake hakuna watu wenye kusema "hatutoki hapa hadi mpokee fomu zetu"? Ni upinzani gani huu!

Haya ni baadhi tu ya maswali yangu kwa sababu tusije kuwalaumu ama wagombea na wale watia nia au wasimamizi. Tujiulize kidogo CDM inawajibika vipi kuwandaa wagombea wake maana msipojibu maswali haya mtakutana tena 2020 na mambo yale yale.

Pendekezo Moja: CDM ije na sera ya wazi na maelekezo ya wazi kuwa wagombea wake wote wahakikishe wanarudisha fomu siku tano kabla ya mwisho wa siku iliyowekwa. Mtashangaa tofauti itakuwa nini hapa.
 
Kwanini kanunu ziwe mpya sio zilizotumika 2014?

Kwanini watendaji waitwe Ikulu mwezi kabla ya uchaguzi?

Kwanini mpaka leo Mbowe ana kesi ya kujibu baada ya kutaka haki itendeke kwenye uchaguzi wa Kinondoni? Wewe uelewi chochote kinachoendea Tanzania bora ungenyamaza tu.

Eti Ccm ambayo inaongoza kwa mbumbumbu imeweza kujaza form halafu vyama vingine vyote wameshindwa ayo maneno uliyoandika waambie wapumbavu tu ndio watakuelewa.
 
Wewe lizee hovyo sana ulitaka warudishe wapi form wakati watendaji walikuwa mafichoni kuwajazia wagombea wa ccm?

Kwani CHADEMA ni mara yao ya kwanza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa?

Ni kwanini wagombea wa vyama vya upinzani tu ndiyo wameenguliwa kwenye uchaguzi ?

Hivi unataka kusema kwamba wagombea wa chadema wameenguliwa kwa uzembe wa chama ?

Kifupi wewe mzee unazeeka vibaya. Nasikitika sana kuwahi kupoteza muda wangu takribani 6 years nikisoma makala zako magazetini.
 
Maswali haya naona yanahusu hata ACT Wazalendo... ni katika kuelewa masuala ya upinzani hasa kwenye mazingira ambayo wanajua kabisa hawawezi kutendewa kwa haki.
 
Kwanini kanunu ziwe mpya sio zilizotumika 2014?
Kwanini watendaji waitwe ikulu mwezi kabla ya uchaguzi?
kwanini mpaka leo Mbowe ana kesi ya kujibu baada ya kutaka haki itendeke kwenye uchaguzi wa kinondoni?

Miaka haigandi; kwani kabla ya 2014 watu walikuwa hawaenguliwi? au 2014 wagombea wote wa upinzani walipitishwa? Au mmeshasahau?
 
Mzee una habari kuwa ACT ilikuwa na watu 173,593 walioomba kugombea kwenye serikali za mitaa lakini kati yao watu 166,649 Wameenguliwa, yaani 96% ya waliogombea kupitia ACT wameenguliwa je unalijua hilo?

Je una habari kuwa 97% ya waliotaka kugombea kupitia Chadema wameenguliwa?

Mzee una habari kuwa watu wote walioomba kugombea kupitia NCCR-Mageuzi katika wilaya ya Vunjo wameenguliwa?

Mzee Mwanakijiji acha kulaumu Victim, usishiriki karamu ya uonevu na udhalimu wa ajabuajabu, wewe ni mtu mzima achana na habari hizi mbofumbofu!
 
Yaan mkuu huoni kilichofanyika?...waru kunyimwa.haki makisudi na waziwazi...?
Siku hizi umekuwaje...yaan na akili zako hizo unaona ni kosa chadema..kwamba wagombea asilimia 90 walioenguliwa walikiwa hawazijui taratibu?..real!?...
 
Maswali haya naona yanahusu hata ACT Wazalendo... ni katika kuelewa masuala ya upinzani hasa kwenye mazingira ambayo wanajua kabisa hawawezi kutendewa kwa haki.
Maswali ya kipumbavu. hv unaishi Tanzania kweli?Hakuna technical zilizojitokeza ni uhuni mtupu wa CCM na serkali yake. Achana na na hoja za kitoto. Nyambafu
 
Back
Top Bottom