Ccm ambayo inaongoza kwa mbumbumbu imeweza kujaza form halafu vyama vingine vyote wameshindwa ayo maneno uliyoandika waambie wapumbavu tu ndio watakuelewa.
Mkuu hapo kwenye maandishi yaliyokolezwa ni mtazamo au hisia zako tu, unaweza usiwe sahihi.
Una kipimo gani cha kusema hivyo?
Ushahidi unaonesha CCM maeneo mengi wameweka watu wenye elimu kubwa au elimu ya juu wakati upinzani wameweka vijana wenye elimu ndogo ila ni maarufu.
Unakuta huyo wa CCM ameshashika nyadhifa kubwa hata mkuu wa chuo cha elimu ya juu lakini bado CCM wamempa mafunzo juu ya ujazazi fomu za wagombea na namna ya kuendesha kampeni.
Huyo msomi wa CCM unakuta amezowea kujaza nyaraka za serikali n.k.
Mfano huku kwetu Ubungo Msewe mgombea wa CDM ni form 6, ana uzoefu wa kazi za ulinzi, wakati CCM wamemuweka Mzee aliyewahi kuwa mkuu wa chuo cha Takwimu Changanyikeni. Nadhani hapo unaona tofauti kubwa.
Mnakumbuka jambo dogo tu la kujaza fomu ya mchezaji bora wa FIFA ilimuharibia sana Mohamed Salah pale uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Misri walivyojaza kwa herufi kubwa sahihi zao kwenye fomu za kupigia kura. Herufi kubwa au ndogo inaweza kukunyima ushindi kwa kukiuka mashariti.
Dharau na dhana kama zako ndio husababisha viongozi wa upinzani hasa CDM kutokuchukua hatua za makusudi kutoa elimu na mikakati kwa wagombea wao jinsi ya kujaza fomu, kujilinda wasikosee kitu ktk kampeni na kutenguliwa ushindi wao. Hii kujiamini sana bila mipango na mikakati ni kosa la kiufundi.
Mwisho ningependa kuwatetea upinzani hasa CHADEMA kwenye suala la kukatazwa hata mikutano ya ndani kunaweza kuwa kumechangia sana wao kushindwa kutoa mafunzo kwa wagombea wao na wasimamizi kwa gharama nafuu kwa kuwakusanya pamoja badala ya kuzunguka nyumba hadi nyumba au kila kitongoji.
Kwahili la kuzuwia mikutano hadi ya ndani ya wapinzani huku wao wakifanya ni aibu na fedhea kwa serikali na CCM, hamuwezi kujivua lawama za uvurugaji demokrasia. Kwa hili nawaambia historia itawahukumu wote mliohusika hata siku mkitangulia mbele za haki, huku nyuma mtaacha maandishi mengi ya kuwaandika ubaya juu ya jambo hili. Mngeacha tu mikutano ya ndani hakuna baya lingetokea kwa taifa, lakini haya mliyofanya yanapika hatari kubwa ya chuki na uhasi kama wa jirani zetu nchi zilizotuzunguka.