Tatizo la siasa za Kiafrika sii Upinzani wa Sera hata kidogo maana Zitto mwenyewe hukosoa UTEKELEZAJI kutokana na Mavuno. Yaani tukisha fikia mafanikio fulani yeye husema hayatoshi, yeye angefanikisha zaidi. Sasa sielewi utafanikishaje ukiwa nje?Naamini wapo waliozaliwa kuwa wakosoaji wa Sera 'mfu' na naamini pia wapo waliozaliwa kuwa viongozi wakuu au watawala.
Zitto atabaki kuwa mkosoaji mkubwa wa Sera za JPM.
Na sii peke yake, Wanaharakati wote husemea nje ya uwanja, Ukimwambia Maria Sarungi au Fatma Karume waingie Uwanjani wanasema wao sii Wanasiasa ila Wanaharakati.. Harakati gani hujipambanua na Vyama vya Siasa?..
- Miafrika Ndivyo Tulivyo