Habari zenu watafutaji wenzangu! Kama kawaida mimi niko poa sana naendelea na ugunduzi wa mawazo ya biashara ngeni kidogo ila kwenye utekelezaji ndo huwa nateleza kutokana na sababu mbalimbali kama vile kubanwa na kazi, kukosa wasaidizi wenye uwezo mzuri kiuendeshaji, mtaji wa kutosha n.k.
Alfajiri (Muda wangu wa kuwazia maisha) ya jumanne wiki iliyopita nilipata wazo la biashara, nayo si nyingine bali ni Maktaba Binafsi kwa ajili ya vitabu vya aina mbalimbali.
Hapa nimeona kuna fursa ya kupata pesa nyingi na za kudumu kupitia uazimishaji na uuzaji wa vitabu kwa wanafunzi na watu wengine, kwani kutakuwa na vitabu vya masomo ya shule na chuo kwa ngazi zote na pia vitabu vya story, comedy n.k. nje ya masomo ya shuleni au chuo.
Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza upatikanaji wa vitabu na study materials nyingine katika jamii, hivyo kusaidia jamii nzima kwa ujumla.
Kutokana na hayo, nimeianika hapa fursa hii ili kwa mtu yeyote atakayeiona aitathmini na kuichangamkia popote atakapoweza, kwani itasaidia jamii nzima ya watanzania.
Mungu atubariki wajasiriamali na wanaJF wote kwa ujumla!