Wazo jipya la biashara

Wazo jipya la biashara

ELAFU

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2014
Posts
410
Reaction score
150
Habari zenu watafutaji wenzangu! Kama kawaida mimi niko poa sana naendelea na ugunduzi wa mawazo ya biashara ngeni kidogo ila kwenye utekelezaji ndo huwa nateleza kutokana na sababu mbalimbali kama vile kubanwa na kazi, kukosa wasaidizi wenye uwezo mzuri kiuendeshaji, mtaji wa kutosha n.k.
Alfajiri (Muda wangu wa kuwazia maisha) ya jumanne wiki iliyopita nilipata wazo la biashara, nayo si nyingine bali ni Maktaba Binafsi kwa ajili ya vitabu vya aina mbalimbali.
Hapa nimeona kuna fursa ya kupata pesa nyingi na za kudumu kupitia uazimishaji na uuzaji wa vitabu kwa wanafunzi na watu wengine, kwani kutakuwa na vitabu vya masomo ya shule na chuo kwa ngazi zote na pia vitabu vya story, comedy n.k. nje ya masomo ya shuleni au chuo.
Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza upatikanaji wa vitabu na study materials nyingine katika jamii, hivyo kusaidia jamii nzima kwa ujumla.
Kutokana na hayo, nimeianika hapa fursa hii ili kwa mtu yeyote atakayeiona aitathmini na kuichangamkia popote atakapoweza, kwani itasaidia jamii nzima ya watanzania.

Mungu atubariki wajasiriamali na wanaJF wote kwa ujumla!
 
wazo zuri lakini kama vile linahitaji mtaji ulioshiba kidogo kwa haraka haraka. Tusubiri wajuvi wanaweza kutufumbua macho tunalianzaje hili jambo sisi wenye vijisenti...
 
hiyo biashara jitahidi upate location nzuri..inaweza ikakulipa..
 
Utakuwa una-azimisha au utakuwa unafanya watu wasome pale pale (reference..)

Kwa kuazimisha utabana vipi hulka yetu ya watanzania ya kukosa uaminifu na uharibifu.., na kama utakuwa unataka watu wasomee palepale utawa-charge vipi ?

Ingawa unaweza ukawa-charge membership fees na upatikanaji wa vitabu sababu ni service unaweza ukapata vitabu vingi bure kutoka kwa wahisani.., ila sababu wateja wako wengi ni wanafunzi (huenda membership charge ikawawia vigumu kulipa) na sababu ni wengi nadhani utahitaji kujenga / rent jengo kubwa kuwahifadhi hawa watu wote hivyo gharama za kuendeshea zikawa kubwa..

Kwa yote hayo juu utaona kwamba ndio maana library service mara nyingi is service oriented na inaendeshwa na serikali/taasisi sio kwa ajili ya kupata faida..., ila labda unaweza ukaanzisha hii kama Msaada na ikawa inaendeshwa kwa kupata misaada kutoka serikalini na wahisani
 
Back
Top Bottom